Jul 21, 2020 11:31 UTC
  • Hali ya fadhaa kando ya kasri ya kifalme ya Saudi Arabia

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kusikika hii leo milio ya risasi kando ya kasri ya kifalme huko Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia.

Harakati ya Uhuru na Mabadiliko leo imeripoti kuwa, sauti za ufaytuaji risasi zimesikika leo kando ya kasri ya kifalme huko Riyadh wakati huu ambapo Mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz amelazwa katika hospitali ya Mfalme Faisal huko Riyadh nchini humo. 

Japokuwa serikali ya Saudi Arabia imeficha taarifa za kujiri purukushani za ufyatuaji risasi huo hii leo karibu na ikulu ya kifalme huko Riyadh lakini picha za kile kilichojiri zimechapishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Katika upande mwingine, kitendo cha kupelekwa hospitali usiku Mfalme Salman kimewafanya weledi wa mambo wazingatie pakubwa suala hilo; kiasi kwamba baadhi ya wafanyakazi wa serikali wamesema katika mitandao ya kijamii kuwa, Mfalme Salman amepelekwa hospitali licha ya ikulu hiyo ya kifalme kuwa na suhula za tiba za kisasa. Inaonekana kuwa, purukushani zinazoripotiwa kujiri huko Saudi Arabia zinahusiana na vuta nikuvute ndani ya ukoo wa kifalme kwa ajili ya kuwania madaraka; huku kukiwa pia na tetesi za kuaga dunia Salman bin Abdulaziz. 

Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia aliye mahututi  

Shirika rasmi la habari la Saudi Arabia jana Jumatatu liliinukuu vyanzo vya kasri ya nchi hiyo na kutangaza kuwa Mfalme Salman ameelekea hospitali kutokana na kuwa na matatizo katika kibofu nyongo (GallBladder) na kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.  

Tags