Al-Hashdu-Sha'abi yarejesha usalama kamili kaskazini mwa Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62585-al_hashdu_sha'abi_yarejesha_usalama_kamili_kaskazini_mwa_iraq
Afisa wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashdu Sha'abi ametangaza kuwa wapinagaji wa harakati hiyo wamezuia kujiri matukio ya kiusalama kaskazini mwa Iraq kwa kutekeleza oparesheni za kiusalama na kiintelijinjsia katika siku za karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 03, 2020 03:03 UTC
  • Al-Hashdu-Sha'abi  yarejesha usalama kamili kaskazini mwa Iraq

Afisa wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya al Hashdu Sha'abi ametangaza kuwa wapinagaji wa harakati hiyo wamezuia kujiri matukio ya kiusalama kaskazini mwa Iraq kwa kutekeleza oparesheni za kiusalama na kiintelijinjsia katika siku za karibuni.

Ali al Husseini afisa wa kundi hilo la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq anayehusika na masuala ya usalama kaskazini mwa nchi amesema kuwa, oparesheni za kijeshi za wapiganaji wa al Hashdu Sha'abi mwezi uliopita zimepelekea kudhaminiwa usalama kamili na kusakwa mamluki waliosalia wa kundi la kigaidi la Daesh na kusambaratishwa makazi na maficho yao makuu. 

Al Hussein ameongeza kuwa, kundi la kigaidi la Daesh hivi sasa limedhoofika na halina nguvu; na mamluki waliosalia wa kundi hilo pia wanasakwa kila uchao na wapiganaji wa al Hashdu Sha'abi kwa kushirikiana na askari usalama wengine.  

Masalia ya kundi la kigaidi la Daesh yanaendelea kutekeleza oparesheni za kigaidi katika baadhi ya maeneo ya Iraq licha ya kundi hilo kusambaratishwa mwezi Novemba mwaka 2017. 

Magaidi wa Daesh kabla ya kusambaratishwa huko Iraq 

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq imetangaza kuwa mnamo miezi ya Mei na Juni mwaka huu karibu magaidi 419 wenye mfungamano na Daesh walitiwa mbaroni katika oparesheni ya vikosi vya nchi hiyo na kundi la al Hashdu- Sha'abi.