HAMAS: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni kumhudumia adui Mzayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65292-hamas_kuanzisha_uhusiano_wa_kawaida_na_israel_ni_kumhudumia_adui_mzayuni
Mjumbe mwadamizi wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utwala haramu wa Israel ni kumhudumia adui Mzayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2020 23:17 UTC
  • HAMAS: Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel ni kumhudumia adui Mzayuni

Mjumbe mwadamizi wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, hatua ya baadhi ya mataifa ya Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utwala haramu wa Israel ni kumhudumia adui Mzayuni.

Izzat al-Rishq amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Habari la Palestina la Quds Net na kueleza kwamba, Hamas inayatambua mataifa ya Kirabu na Kiislamu kuwa himaya yake ya kistratejia na kwamba, harakati hii imeweza kulinda na kuhifadhi uhusiano wenye mlingano na mataifa yote yenye kufanya mambo kwa ajili ya kuhudumia amani na kupatikana haki za taifa la Palestina.

Afisa huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ua Kiislamu ya Palestina HAMAS amewataka watawaa wa Kiarabu kutazama upya mahesabu na manufaa ya kweli ili nchi zao zisije kuwa mlango wa kupenya na kuingia adui Mzayuni katika usalama wa Kiarabu na Kiislamu.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS

 

Hivi karibuni, mfalme wa Morocco Mohammed VI alimwarifu Rais Donald Trump wa Marekani kwenye mazungumzo kwa njia ya simu kuwa amekubali kurejesha mawasiliano ya kiserikali na kuanzisha uhusiano wa kibalozi na utawala wa Israel haraka iwezekanavyo.

Itakumbukwa kuwa, tarehe 25 Septemba, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Imarati na Bahrain walisaini mkataba wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel katika hafla iliyofanyika Ikulu ya White House mjini Washington. Sudan pia imefuata mkumbo huo huo na kutangaza utayarifu wa kuanzisha uhusiano na utawala huo bandia, uamuzi ambao umeendelea kulalamikiwa na wapenda haki kote ulimwenguni.