Damascus yakadhibisha kupokea rasimu ya katiba
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7918-damascus_yakadhibisha_kupokea_rasimu_ya_katiba
Serikali ya Syria imekadhibisha taarifa kuwa imetumiwa rasimu ya Katiba mpya na kusema kuwa, Damascus haijapokea rasimu ya aina yoyote kuhusu katiba ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 09:49 UTC
  • Rais Bashar al Assad wa Syria
    Rais Bashar al Assad wa Syria

Serikali ya Syria imekadhibisha taarifa kuwa imetumiwa rasimu ya Katiba mpya na kusema kuwa, Damascus haijapokea rasimu ya aina yoyote kuhusu katiba ya nchi hiyo.

Ofisi ya Rais Bashar al Assad wa Syra leo imetoa taarifa ya kujibu taarifa zilizoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kuwasilishwa rasimu ya katiba mpya ya Syria kwa serikali ya nchi hiyo.

Siku kadhaa zilizopita baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza kuwa Russia imeikabidhi Syria rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais wa Syria imebainisha kuwa, katiba yoyote mpya kwa ajili ya Syria katika siku zijazo haitawasilishwa nje ya nchi, bali itatoka ndani ya Syria kwenyewe na ni Wasyria wenyewe ndio watakaoijadili na kufikia mapatano kuhusu katiba yao hiyo.