Al-Bakhiti: Umoja wa Ulaya umeonyesha kuporomoka kwake kimaadili
(last modified Sat, 19 Mar 2022 11:57:52 GMT )
Mar 19, 2022 11:57 UTC
  • Al-Bakhiti: Umoja wa Ulaya umeonyesha kuporomoka kwake kimaadili

Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen, amekosoa hatua ya Umoja wa Ulaya (EU) ya kuiweka harakati ya Ansarullah katika orodha yake nyeusi na kusema: "EU imeonyesha kuporomoka kwake kimaadili kwa kitendo hiki."

Umoja wa Ulaya (EU) umeiweka harakati ya Ansarullah ya Yemen kwenye "orodha nyeusi" kufuatia mashambulizi yake ya hivi karibuni dhidi ya Saudi Arabia, na umeamua kufunga akaunti za benki za wanachama wa harakati hiyo na kupiga marufuku uhamishaji wao wa fedha.

"Orodha nyeusi" ya EU ilianzishwa mnamo 2014 kwa ajili ya vikwazo dhidi ya vita vya Yemeni.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Mayadeen, Mohammed al-Bakhiti, mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen, amelaani hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiweka Ansarullah katika orodha hiyo. 

Al-Bakhiti ameongeza kuwa, uamuzi wa kuiweka Ansarullah katika orodha nyeusi ya EU umechuliwa huku ikitarajiwa kwamba, baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, umoja huo utarekebisha mwenendo wa maadili yake ya kisiasa.

Mjumbe wa Baraza la Kisiasa la Serikali ya Uokoaji wa Kitaifa ya Yemen amesema kuwa, jeshi la Yemen na kamati za wananchi zitaendelea kufanya kazi ya kulinda ardhi yote ya nchi yao. 

Katika kukabiliana na jinai za muungano vamizi wa Saudi Arabia na Imarati, jeshi la Yemen na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah wamekuwa wakilenga maeneo ya kistratijia ndani kabisa ya Saudi Arabia na Imarati.

Tags