Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Mustakabali wa kutisha utaziandama nchi vamizi
(last modified 2022-03-23T07:48:42+00:00 )
Mar 23, 2022 07:48 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa Yemen: Mustakabali wa kutisha utaziandama nchi vamizi

Waziri wa Ulinzi wa serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen amesisitiza kuwa, muundo na sura ya muqawama katika siku zijazo utakuwa wa kutisha kwa nchi vamizi.

Muhammad al Aatifi ameeleza kuwa, mwaka wa nane wa kusimama imara na kwa uthabiti wananchi wa Yemen, ni mwaka wa dhoruba na tufani za Yemen, wa mafanikio makubwa ya silaha za kisasa za kistratejia na ni mwaka wa uchukuaji hatua kali na madhubuti zaidi za kuzuia hujuma dhidi ya nchi hiyo.

Al Atifi ameongezea kwa kusema: "leo sisi tumo kupiga hatua thabiti zaidi mbele kwa ajili ya kupata mafanikio mapya ya kijeshi, ambayo yatakuwa ya kustaajabisha; mafanikio ambayo yatageuza mlingano wa nguvu."

Wakati huohuo, Muhammad al Bukhayti, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen ameashiria operehseni zijazo za kijeshi za muqawama wa nchi hiyo dhidi ya ngome za Saudi Arabia na kusisitiza kuwa, mashambulio ya muqawama wa Yemen katika siku zijazo yataiumiza mno nchi hiyo na kwamba muqawama huo utaendelea kuzilenga taasisi za mafuta za ndani ya ardhi ya Saudia.

Muhammad al Bukhayti,

Usiku wa kuamkia Jumatatu, kikosi cha ndege zisizo na rubani na makombora cha jeshi la Yemen na wapiganaji wa kujitolea kilishambulia kwa makombora ya balestiki miundomsingi ya kiuchumi, kijeshi na viwanda ya utawala wa Aal Saud kikiwemo kiwanja cha ndege na kiwanda cha kusafisha mafuta cha Jeddah.

Jumamosi usiku pia, jeshi la Yemen lilishambulia  kwa makombora kadhaa ya balestiki na droni taasisi kadhaa muhimu za Saudia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ukiwemo mji mkuu Riyadh.../

Tags