Mbunge wa Lebanon: Hizbullah inatekeleza majukumu yake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i82102-mbunge_wa_lebanon_hizbullah_inatekeleza_majukumu_yake
Mbunge wa Lebanon ameashiria uchaguzi ujao wa bunge nchini humo na kueleza kuwa harakati ya muqawama ya Hizbullah inaheshimu na kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na migogoro na majanga mbalimbali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 03, 2022 06:57 UTC
  • Mbunge wa Lebanon: Hizbullah inatekeleza majukumu yake

Mbunge wa Lebanon ameashiria uchaguzi ujao wa bunge nchini humo na kueleza kuwa harakati ya muqawama ya Hizbullah inaheshimu na kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na migogoro na majanga mbalimbali.

Rais Michel Aoun wa Lebanon ametoa dikrii na kutangaza kuwa, uchaguzi wa bunge la nchi hiyo uafanyika Mei 15 mwaka huu. Hassan Izzudin mbunge wa Lebanon ambaye ni mwakilishi wa mrengo wa wenye mfungamano na harakati ya muqawama ya Hizbullah leo ameeleza kuwa: baadhi ya watu waliotawala Lebanon katika miongo kadhaa liyopita na kuiba mali za nchi hiyo  tayari wameandaa orodha ya wapiga kura na baadhi ya wengine ambao leo wanadai kuwa eti wanapambana na ufisadi; wenyewe ndio wanaoongoza kwa ufisadi huko Lebanon.  

Rais wa Lebanon, Michel Aoun 

Izzudin amesisitiza kuwa, harakati ya Hizbullah kamwe haitakwepa jukumu lake la kufanya juhudi za kutatua migogoro ya ndani huko Lebanon; sawa kabisa ambavyo hivi sasa inaheshimu na kutekeleza majukumu yake katika kupambana na utawala wa Kizayuni. 

Sheikh Nabil Qawooq mwakilishi wa Baraza Kuu la Hzbullah aliwahi kusema kuwa, baada ya nchi ajinabi kugonga mwamba katika vikwazo vyao vikubwa dhidi ya Hizbullah; na wakati huo huo kushindwa katika nyanja za kijeshi na kiusalama dhidi ya nchi hiyo hvi sasa zimekodisha balozi zao ili kueneza chuki dhidi ya Hizbullah.