Saudia imeiba mafuta ya Yemen yenye thamani ya dola bilioni 9
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i87286-saudia_imeiba_mafuta_ya_yemen_yenye_thamani_ya_dola_bilioni_9
Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imesema Saudi Arabia na washirika wake wameiba mafuta yenye thamani ya mabilioni ya dola tangu waivamie nchi hiyo maskini ya Kiarabu mwaka 2015.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 21, 2022 23:54 UTC
  • Saudia imeiba mafuta ya Yemen yenye thamani ya dola bilioni 9

Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imesema Saudi Arabia na washirika wake wameiba mafuta yenye thamani ya mabilioni ya dola tangu waivamie nchi hiyo maskini ya Kiarabu mwaka 2015.

Waziri wa Mafuta na Madini wa Yemen, Ahmad Abdullah Dares amesema kati ya mwaka 2018 na Julai mwaka huu, muungano vamizi wa Saudia umeiba mapipa milioni 130 ya mafuta ya Yemen, yenye thamani ya dola bilioni 9.5.

Amesema muungano huo vamizi uliiba mapipa milioni 29.6 ya mafuta ya Wayemen mwaka 2019, na mapipa milioni 31 mwaka jana 2021 yaliyokuwa na thamani ya dola bilioni 2.3.

Maafisa wa Yemen wametahadharisha kwamba, endapo akiba ya bidhaa za mafuta ya nchi hiyo itamalizika, sekta nyingi zitasita kufanya kazi kikamilifu na maafa makubwa yatatokea nchini humo.

Meli za Saudia zinavyoiba mafuta katika Bandari ya Yemen

Mwezi uliopita, Essam al-Mutawakel, Msemaji wa Shirika la Mafuta ya Petroli la Yemen (YPC) alisema nchi hiyo ina rasilimali ya kutosha ya mafuta ghafi ya gesi ya kuweza kutosheleza mahitaji ya ndani na hata kuuza nje ya nchi. 

Mbali na wizi ya mafuta, muungano huo vamizi unafanya magendo ya athari za kale za Yemen na kuziuza kwenye soko la Ulaya kupitia Saudi Arabia.