Msimamo mmoja wa wapinzani Bahrain wa kususia uchaguzi wa Bunge
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i87618-msimamo_mmoja_wa_wapinzani_bahrain_wa_kususia_uchaguzi_wa_bunge
Uchaguzi wa Bunge nchini Bahrain umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Hata hivyo mrengo wa upinzani nchini humo umetangaza kususia uchaguzi huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 30, 2022 21:49 UTC
  • Msimamo mmoja wa wapinzani Bahrain wa kususia uchaguzi wa Bunge

Uchaguzi wa Bunge nchini Bahrain umepangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Hata hivyo mrengo wa upinzani nchini humo umetangaza kususia uchaguzi huo.

Tangu ulipoanza ukandamizaji dhiidi ya vuguvugu la mapambano ya wananchi lililoanza mwaka Februari 14, 2011 hadi sasa, Bahrain imeendelea kushuhudia wimbi kubwa la malalamiko na upinzani wa umma unaotaka marekebisho ya kisiasa yafanyike nchini humo.  Katika kipindi chote hiki kunashuhudiwa makabiliano baina ya wanajeshi wa utawala wa Aal Khalifa na wananchi. Katika hali ambayo, utawala wa Aal Khalifa katika kipindi cha miaka 11 iliyopita, haujaheshimu haki yoyote ile ya wananchi wa nchi hiyo iwe ya kisiasa au ya kiraia, hivi sasa unataka kufanyike uchaguzi mpya wa Bunge.

Utawala wa Aal Khalifa unalenga mambo mawili katika kuitisha uchaguzi huo wa Bunge:

Mosi, unataka kuonyesha kwamba, licha ya kuweko malalamiko ya wananchi kwa miaka 11, lakini ungali una uhalali wa kisheria wa kuendelea kuweko madarakani. Hii ni katika hali ambayo, hakuna mpinzani au mkosoaji yeyote yule wa utawala wa Aal Khalifa ambaye ana nia ya kushiriki katika uchaguzi ujao wa Bunge. Hii ni kutokana na kuwa, wapinzani hao wanaamini kwamba, kimsingi utawala huo hauna uhalali wa kisheria. Kwa msingi huo, kuanzia sasa tunaweza kutaraji kwamba, ushiriki katika uchaguzi huo utakuwa wa kiwango kidogo kabisa na hivyo kuwa ushahidi wa wazi wa kutokuwa na uhalali wa kisheria utawala wa kifalme wa Aal Khalifa.

Ukandamizaji wa vikosi vya usalama vya Bahrain

 

Lengo la pili linalofuatiliwa na utawala wa Aal Khalifa kuitisha uchaguzi huo wa Bunge ni kuhakikisha kuwa, mzunguko wa uchaguzii nchini humo hausimami. Bahrain ni miongoni mwa mataifa machache ya Kiarabu ambayo yana historia ya mfumo wa kiraia. Uchaguzi wa Bunge ulikuwa ukifanyika nchini Bahrain tangu katika miaka ya awali ya nchi hiyo kupata uhuru yaani muongo wa 70. Lakini baada ya hapo, ukafutwa kwa takribani miongo mitatu. Hata hivyo baada ya kuanza karne mpya, uchaguzi wa Bunge haukusimamishwa. Licha ya kuwa uchaguzi huo ni wa kimaonyesho tu, lakini umekuwa ukifanyika. Utawala wa Aal Khalifa unataka kufikisha ujumbe huu kwamba, licha ya kuweko malalamiko, lakini chaguzi zimekuwa zikifanyika nchini humo. Ukweli wa mambo ni kuwa, lengo la uchaguzi huo siyo kuwa kigezo katika kuundwa serikali, bali jambo hilo lina umuhimu kwa ajili ya kujipigia debe kisiasa utawala wa Aal Khalifa.

Wapinzani wa utawala wa Aal Kkhalifa nao wana sababu kadhaa muhimu za kususia uchaguzi huo.

Sababu ya kwanza ni kuwa, utawala wa Aal Khalifa hauna uhalali wa kisheria na wanaamini kwamba, hata uchaguzi wenyewe wa Bunge ni wa kimaonyesho tu, na lengo lake ni kuzihadaa fikra za waliowengi ulimwenguni.

Kuhusiana na hilo, Harakati ya al-Wafaa al-Islami moja ya makundi ya upinzani na yanayoukosoa utawala wa Aal Khalifa nchini Bahrain imetoa taarifa ambapo sambamba na kutangaza kususia uchaguzi ujao wa Bunge wa nchi hiyo imesema bayana kwamba, kususia uchaguzi huo ni moja ya mbinu muhimu za kuzipokonya uhalali tawala za kitaghuti.

 

Sababu ya pili ni kuwa, wakosoaji na wapinzani nchini Bahrain wanaamini kuwa, hadi sasa Bunge la nchi hiyo halijafanya kitu chochote cha maana katika mfumo wa siasa za nchi hiyo. Bunge hilo limeshindwa hata kutekeleza jukumu lake muhimu la kutunga sheria, kwani mfumo unaotawala nchini humo ni wa kidikteta na Bunge liko katika udhibiti wa utawala. Hivyo, kabla ya kitu chochote, Bunge la Bahrain ndilo linalounga mkono sera za ukandamizaji za utawala wa ukoo wa Aa Khalifa.

Sababu ya tatu ni kwamba, kushiriki uchaguzi ni kuthibitisha mfumo wa kidiktea na ukandamizaji nchini Bahrain, na ni kinyume kabisa na maslahi ya wananchi. Kuhusiana na hilo, Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa Mapinduzi ya Wananchi wa Bahrain sanjari na kutoa taarifa ya kususiwa uchaguzi ametangaza kuwa, uchaguzi ujao ni bandia na uongo mtupu ambao unapuuza na kufumbia macho haki za wananchi. Utekelezwaji wa mchakato wa uchaguzi umefanyika kwa msingi wa Ramani ya Njia ya Kidhalimu ya utawala wa Aal Khalifa na hilo linafanyika katika fremu ya kutekeleza malengo ya kidikteta na ya upande mmoja ambayo kimsingi ni kinyume kabisa na maslahi ya wananchi,

Kwa kuzingatia sababu hizo, kususia ni moja ya nyenzo kuu za wapinzani ambao wanaunda sehemu kubwa ya wakazi wa Bahrain, wenzo ambao wameuweka kama mkakakati wao wa kukabiliana na uchaguzi ujao wa Bunge nchini humo.