Msimamo imara wa muqawama wa Lebanon wawapigisha magoti Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89252-msimamo_imara_wa_muqawama_wa_lebanon_wawapigisha_magoti_wazayuni
Baada ya Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel kukubaliana na mpango wa kuchorwa mipaka ya baharini baina ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika makala chini ya kichwa cha maneno: "Ushindi wa Hizbullah katika Mapatano."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 13, 2022 23:07 UTC
  • Msimamo imara wa muqawama wa Lebanon wawapigisha magoti Wazayuni

Baada ya Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel kukubaliana na mpango wa kuchorwa mipaka ya baharini baina ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni, gazeti la Kizayuni la Haaretz limeandika makala chini ya kichwa cha maneno: "Ushindi wa Hizbullah katika Mapatano."

Gazeti hilo limekiri kwamba utawala wa Kizayuni umelazimika kukubali kutia saini makubaliano hayo kwani hauna uwezo wa kuingia vitani na Lebanon na hasa Hizbullah na iwapo vita vitatokea basi yatakuwa ni majuto makubwa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa upande wao, viongozi wa Palestina wanasema, kama Hizbullah isingeliingia katika suala la kuchorwa mipaka hiyo ya baharini, Lebanon ingelidhulumiwa sana. Lakini baada ya Hizbullah kutishia kutumia nguvu za kijeshi kusimamisha uchimbaji wowote wa gesi katika eneo hilo, Marekani imelazimika kuja na mpango ambao unalinufaisha taifa la Lebanon.

Karish

 

Katika hotuba yake ya hivi karibuni, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah alisema, iwapo Lebanon itanyimwa haki yake ya kufaidika na mafuta na gesi yake, basi hakuna yeyote atakayeweza kuchimba gesi katika medani ya Karish. 

Viongozi wa Palestina wamesema, kuna mambo mbalimbali yamewalazimisha Wazayuni kukubaliana na mipaka hiyo mipya ikiwa ni pamoja na onyo la Hizbullah na msimamo imara wa serikali ya Lebanon wa kuwa kwake pamoja na Hizbullah katika suala hilo zima. 

Mambo hayo yalitia kasi mazungumzo kuhusu mipaka hiyo mipya baina ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Onyo la Hizbullah liliilazimisha Marekani kuingilia kati na kutoa mapendekezo ambayo awali yalikataliwa na serikali ya Beirut mpaka Washington ikalazimika kuyafanyia marekebisho kwa manufaa ya  Lebanon. Hatimaye utawala wa Kizayuni nao umelazimika kukubaliana na mpango huo.