Raia wengine 15 wakiwemo watoto 8 wahukumiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i89918-raia_wengine_15_wakiwemo_watoto_8_wahukumiwa_kunyongwa_nchini_saudi_arabia
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Kisaudia lenye makao yake barani Ulaya limefichua kuwa, viongozi wa Riyadh wamewahukumu adhabu ya kunyongwa wafungwa 15 wa kisiasa wakiwemo watoto kadhaa wadogo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2022 22:59 UTC
  • Raia wengine 15 wakiwemo watoto 8 wahukumiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Kisaudia lenye makao yake barani Ulaya limefichua kuwa, viongozi wa Riyadh wamewahukumu adhabu ya kunyongwa wafungwa 15 wa kisiasa wakiwemo watoto kadhaa wadogo.

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Kisaudia lenye makao yake barani Ulaya limeunuuku mtandao wenye kufichua mambo wa Saudi Leaks na kutangaza kuwa, kutolewa hukumu ya wafuungwa hao wa kisiasa kunaifanya idadi ya watuu wanaokabiliwa na hatima ya kunyongwa kufikia 53 wakiwemo watoto wanane.

Tokea kuanza mwaka huu wa 2022 hadi sasa, Saudi Arabia imewanyonga na kuwatia kitanzi watu 121.

Kesi 81 za watu kunyongwa kwa umati zimeripotiwa nchini humo; hali ambayo inatajwa kuwa mbaya zaidi ya watu kunyongwa kwa umati katika historia. Watu 41 kati ya hao walionyongwa walikuwa wapinzani ambao ni Waislamu wa madhehebu ya Shia wa nchi hiyo na wenyeji wa maeneo ya Al-Ahsa na Qatif mashariki mwa Saudi Arabia.

 

Tukio kama hilo la kunyongwa idadi hiyo kubwa ya Waislamu wa Kishia huko Saudia katika kipindi cha siku moja lilikuwa halijawahi kushuhudiwa nchini humo.

Takwimu zinazotolewa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu zinaonyesha kuwa, Saudi Arabia imewanyonga watu 1,100 katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Madola yanayodai kuwa vinara wa haki za binadamu ulimwenguni yamenyamazia kimya ukandamizaji na vitendo vya kunyongwa kiholela wapinzani nchini Saudi Arabia.