Uchaguzi wa Bahrain; Wabahrain wanataka haki ya kuainisha mustakbali wao
Katibu Mkuu wa Harakati Ukombozi wa Bahrain amesema kuwa wananchi wa Bahrain wanataka haki zao za kisheria ikiwemo haki ya kuainisha mustakbali wao kupitia harakati yao ya amani.
Uchaguzi wa Bunge la Bahrain umepangwa kufanyika tarehe 12 mwezi huu na wanamapinduzi wa nchi hiyo wameazimia kususia zoezi hilo. Hii ni kwa sababu, uchaguzi huo hauko huru na hauna maslahi kwa watu wa Bahrain.
Abdul Rauf al Shayeb, Katibu Mkuu wa Harakati Ukombozi wa Bahrain amesema: Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa na uhuru wa kuainisha mustakbali wao na kuwachagua watawala wawatakao kwa mujibu wa Katiba. Al Shayeb amesisitiza kuwa, harakakati za kisiasa za kisheria za wananchi wa Bahrain zimekandamiwza ili utawala wa Al Khalifa usalie madarakani na kwamba wananchi wa Bahrain wanaendelea kusisitiza haki yao ya kuainisha mustakbali wa nchi yao.
Katibu Mkuu wa Harakati Ukombozi wa Bahrain ametlia mkazo nafasi muhimu ya wananchi katika uchaguzi wa Bunge na kuwachagua viongozi kwa mujibu wa sheria na kusema: Wananchi wa Bahrain wanapasa kuwa na haki ya kuwachagua viongozi wawatakao.
Abdul Rauf al Shayeb ameongeza kuwa, Katiba ya Bahrain inapasa kuidhinishwa na wananchi na si ile inayoendeleza dhulma na ukandamizaji na kuanzishqa uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel
Tangu Februari 14 mwaka 2011 Bahrain imekumbwa na vuguvugu la harakati za mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa ukoo wa Al Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutekelezwa uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kuingia madarakani serikali itakayochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.