Umaskini waathiri zaidi ya robo ya jamii katika nchi za Kiarabu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) amesema kuwa umaskini umeathiri zaidi ya robo ya jamii katika nchi za Kiarabu.
Ahmed Aboul Ghait amesema kuwa zaidi ya robo ya watu katika nchi za Kiarabu wamekumbwa na umaskini kutokana na janga la corona na taathira zake. Aboul Ghait amesema haya katika mdahalo uliofanyika huko Misri kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika fremu ya shuguli za Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi chini ya anwani ya "Usalama wa Chakula". Mdahalo huo umehudhuriwa na viongozi wa nchi kadhaa na taasisi za kimataifa.
Mwezi Septemba mwaka huu Katibu Mkuu wa Arab League alitahadharisha katika hafla ya ufunguzi wa "Mkutano wa Mazingira na Ustawi 2022" huko Cairo kwamba: hali ya usalama wa chakula katika nchi za Kiarabu inapungua kwa kiasi cha kutia wasiwasi.
Janga la corona duniani limesababisha watu milioni 163 kuishi chini ya mstari wa umaskini.