Ayatullah Issa Qassim: Lengo la Uchaguzi wa Bahrain ni kuua demokrasia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i90332-ayatullah_issa_qassim_lengo_la_uchaguzi_wa_bahrain_ni_kuua_demokrasia
Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kidini wa mapinduzi ya Bahrain amesema kuwa, kususia uchaguzi ujao nchini humo ni hatua inayolenga kulinda demokrasia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 10, 2022 04:14 UTC
  • Ayatullah Issa Qassim: Lengo la Uchaguzi wa Bahrain ni kuua demokrasia

Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kidini wa mapinduzi ya Bahrain amesema kuwa, kususia uchaguzi ujao nchini humo ni hatua inayolenga kulinda demokrasia.

Kiongozi huyo wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia nchini Bahrain amesisitiza kuwa, madai ya viongozi wa utawala wa Bahrain kwamba, uchaguzi ujao wa Bunge katika nchi hiyo unalenga kuimarisha demokrasia hayana ukweli na ni urongo mtupu.

Sheikh Issa Qassim amehoji kwa kusema, vipi uchaguzi huo utakuwa ni wa kuamrisha demokrasia ilihalii utawala huo umewafungia milango watu ambao wanapigania demokrasia? je huku ni kuimarisha demokrasia au ni kuiua?

Kiongozi huyo ambaye amekuwa akisisitiza na kuwataka wananchi wa Bahrain kuusuia uchaguzii huo amenukuliwa mara kadhaa akieleza kwamba, uchaguzi ujao wa Bunge nchini humo hauna lengo jingine isipokuwa kuimarisha mienendo ya kiimla na kidikteta ya watawala wa Aal-Khalifa.

 

Kabla ya hapo pia, mrengo mkubwa zaidi wa upinzani nchini humo ulitangaza kususia uchaguzi huo. Chama cha Kiislamu cha al-Wifaq kimetoa mwito kwa Wabahrain kususia uchaguzi wa Bunge nchini Bahrain.

Uchaguzi wa Bunge la Bahrain umepangwa kufanyika tarehe 12 mwezi huu na wanamapinduzi wa nchi hiyo wameazimia kususia zoezi hilo.

Tangu Februari 14 mwaka 2011 Bahrain imekumbwa na vuguvugu la harakati za mapinduzi ya wananchi dhidi ya utawala wa ukoo wa Al Khalifa. Wananchi wa Bahrain wanataka kuwa huru, kutekelezwa uadilifu, kukomeshwa ubaguzi na kuingia madarakani serikali itakayochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.