Israel kujenga ukuta wa chini ya ardhi huko Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9409-israel_kujenga_ukuta_wa_chini_ya_ardhi_huko_ghaza
Israel inajiandaa kujenga ukuta mkubwa wa saruji huko Ukanda wa Ghaza. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 17, 2016 23:58 UTC
  • Israel kujenga ukuta wa chini ya ardhi huko Ghaza

Israel inajiandaa kujenga ukuta mkubwa wa saruji huko Ukanda wa Ghaza. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth

Gazeti hilo limeeleza kuwa mpango huo wa Israel umekusudiwa kuzuia kile kilichotajwa na utawala wa Kizayuni kuwa ni vitisho vya njia za chini ya ardhi zilizoanzishwa na harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas inayoongoza huko Ghaza.

Ukuta huo ambao utakuwa na urefu wa kilomita 96 utagharimu dola zinazokadiriwa milioni 568. Harakati ya Hamas inasema kuwa njia za chini kwa chini zinahitajika ili kuilinda Ghaza dhidi ya mashambulizi ya Israel. Aidha njia hizo zinatumiwa na raia wa Kipalestina wa Ukanda wa Ghaza kupitishia bidhaa zao za mahitajio.