Saudia yakariri wito wake kwa Marekani kuishambulia kijeshi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9421-saudia_yakariri_wito_wake_kwa_marekani_kuishambulia_kijeshi_syria
Kwa mara nyingine tena utawala wa Saudi Arabia umeitaka Marekani kuishambulia kijeshi Syria na kusisitiza kuwa mashambulizi ya anga dhidi ya majengo ya serikali ndo yataweza kumuondoa mamlakani Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 18, 2016 02:30 UTC
  • Saudia yakariri wito wake kwa Marekani kuishambulia kijeshi Syria

Kwa mara nyingine tena utawala wa Saudi Arabia umeitaka Marekani kuishambulia kijeshi Syria na kusisitiza kuwa mashambulizi ya anga dhidi ya majengo ya serikali ndo yataweza kumuondoa mamlakani Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.

Adel al-Jubeir, Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala wa Aal-Saud aliwaambia waandishi wa habari jana Ijumaa katika ubalozi wa Saudia mjini Washington kuwa, tangu kuibuka kwa mgogoro wa Syria, Riyadh imekuwa ikisistiza kuwa kushambuliwa kijeshi nchi hiyo ya Kiarabu kwa shabaha ya kumuondoa mamlakani Rais Assad ndiyo dawa mjarabu ya kumalizi mzozo huo. Amesema: "Sera madhubuti kama vile mashambulizi ya anga, kutoruhusiwa ndege katika anga ya nchi hiyo sambamba na safari ya ardhini ni katika mambo ambayo Riyadh imekuwa ikiyasisitizia kwa lengo la kumuondoa mamlakani Assad." Kauli ya Jubeir inajiri siku chache baada ya viongozi waadamizi wa serikali ya Washington kutoa wito kama huo. Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal la nchini Marekani maafisa wa Washington walitia saini hivi karibuni waraka wa kutaka maeneo ya serikali ya Damascus yashambuliwe. Gazeti hilo lilifichua kwamba waraka huo rasmi ulitiwa saini na maafisa 51 wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani. Muungano wa kijeshi uliobuniwa na Marekani na nchi waitifaki umekuwa ukilaumiwa kwa kushabulia na kuua kiholela raia wa Syria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa Daesh tokea Septemba mwaka 2014.