Saudia, baba wa kiroho wa magaidi wa ISIS
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9550-saudia_baba_wa_kiroho_wa_magaidi_wa_isis
Mbunge mmoja wa Iran amesema, Saudi Arabia ni baba wa kiroho wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 19, 2016 10:11 UTC
  • Saudia, baba wa kiroho wa magaidi wa ISIS

Mbunge mmoja wa Iran amesema, Saudi Arabia ni baba wa kiroho wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh.

Mohammad Javad Jamali Nubandegi, Mjumbe wa Kamati ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Iran ameashiria taarifa ya pamoja ya Marekani na Saudia dhidi ya Iran. Katika taarifa hiyo ilidaiwa kuwa eti Iran inatekeleza sera haribifu katika eneo. Mbunge huyo mwandamizi Iran amesema: "Hillary Clinton, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Marekani amekiri katika kitabu chake kuwa Marekani ilihusika katika kujitokeza kundi la kigaidi la ISIS. Kwa hivyo kuitaja Iran kuwa eti ni nchi ya kigaidi ni mbinu inayotumiwa kujaribu kukwepa lawama."

Javad Jamali amesema Marekani na Saudi Arabia ndio wahusika wakuu katika kusababisha machafuko na mizozo Mashariki ya Kati. Ameongeza kuwa hivi sasa Iran imeibuka kama dola lenye nguvu katika eneo hili lenye misukosuko.

Javad Jamali amesema, Saudia ina kiburi na ujeuri mkubwa kutokana na utajiri wake na inajitazama kama kiranja wa eneo. Ameongeza kuwa Iran inaunga mkono uthabiti na udugu baina ya nchi za eneo la Mashariki ya Kati.