UN: Zaidi ya madaktari na wauguzi 700 wameuawa Syria
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa madaktari na wauguzi zaidi ya 700 wameuawa nchini Syria tangu nchi hiyo iliposhambuliwa na mamluki wanaosaidiwa na nchi kadhaa za kigeni miaka mitano iliyopita.
Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayochunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Syria, Paulo Pinheiro amelaani mashambulizi yanayolenga hospitani na vituo vya afya nchini Syria na kusababisha maafa kwa raia. Amesema sambamba na kuongezeka idadi ya wahanga wa vita nchini Syria, idadi ya hospitali na wahudumu wa afya inaendelea kupungua, suala ambalo linazidisha mashaka ya kupatikana matibabu. Ameongeza kuwa zaidi ya madaktari na wahudumu wa tiba wameuawa katika mashambulizi yanayolenga vituo vya afya nchini Syria.
Katika upande mwingine afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesema kamati yake inachunguza suala la kutumiwa watoto wadogo kama wapiganaji katika safu za makundi ya kigaidi yanayofanya mashambulizi dhidi serikali ay Syria katika mkoa wa Aleppo.
Paulo Pinheiro amesema kuna ripoti kwamba kundi la Jabhatu Nusra na makundi mengine yanayoshikamana na kundi la Daesh yamesajili mamia ya watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka 15 katika eneo Edlib.