HAMAS: Hatutaruhusu mipango michafu ya Wazayuni itekelezwe Masjidul-Aqswa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i97526-hamas_hatutaruhusu_mipango_michafu_ya_wazayuni_itekelezwe_masjidul_aqswa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, katu haitaruhusu mipango na njama chafu za Wazayuuni dhidi ya msikitii wa al-Aqswa zitekelezwa kivitendo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 18, 2023 22:55 UTC
  • HAMAS: Hatutaruhusu mipango michafu ya Wazayuni itekelezwe Masjidul-Aqswa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, katu haitaruhusu mipango na njama chafu za Wazayuuni dhidi ya msikitii wa al-Aqswa zitekelezwa kivitendo.

Taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeuonya utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel kuhusiana na hatua yoyote yenye nia mbaya dhidi ya msikiti huo mtakatifu.

Tamko hilo la Hamas linafuatia hujuma na uvamiz wa walowezi wa Kizayuni katika msikiti wa al-Aqswa ambao wamekuwa wakiungwa mkono na kupatiwa himaya na jeshii la utawala ghasibu wa Israel.

Katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno sambamba na njama za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa eneo hilo takatifu.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

Walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakivamiia mara kwa mara msikiti wa al-Aqswa na kufanya vitendo vya kichochezi

 

Vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu huko Palestina vinafanyika katika hali ambayo, viongozi wa nchi za Kiarabu na jamii ya kimataifa wameendelea kunyamaza kimya na kutochukua hatua zozote za maana za kukabiliana na vitendo hivyo vinavyokinzana na utu na ubinadamu.

Utawala wa Kizayuni ambao unaungwa mkono kikamilifu na Marekani katika hatua zake hizo haramu umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina; ili kuyazayunisha maeneo hayo na kuhakikisha unazihodhi na kuzidhibiti kikamilifu ardhi za Wapalestina.