-
Ulinzi wa Raia Gaza: Miili 8,000 ya mashahidi wa mauaji ya kimbari bado imefunikwa na vifusi
Feb 14, 2026 02:51Idara ya Ulinzi wa Raia katika Ukanda wa Gaza inasema kuwa maelfu ya miili ya Wapalestina waliouawa katika mashambulizi ya Israel bado imezikwa chini ya magofu ya majengo yaliyoharibiwa katika eneo hilo la Palestina, huku timu za uokoaji zikijitahidi kufika kwenye vitongoji vilivyoharibiwa wakati wa vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Israel.
-
Al Houthi: Iran ni ngome imara inayokwamisha njama za Marekani na Israel
Feb 14, 2026 00:44Kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen amesema kuwa Marekani na Utawala wa Israel zinakabiliana na Iran kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasimama kama kizuizi dhidi ya mradi wao mpana wa kutawala eneo la Asia Magharibi.
-
Chama cha Jamaat-e-Islami nchini Bangladesh chatilia shaka matokeo ya uchaguzi
Feb 13, 2026 22:53Chama cha Jamaat-e-Islami, chama kikubwa zaidi cha Kiislamu nchini Bangladesh, kimehoji matokeo ya uchaguzi uliofanyika nchini humo majuzi, ambapo kimeshika nafasi ya pili kwa kupata viti 74 baada ya Chama cha Kizalendo cha Bangladesh, ambacho kumeshinda viti 212 kati ya 300 vya Bunge.
-
Iran yalaani juhudi za Israel za kunyakua Ukingo wa Magharibi, yasema ni 'maangamizi ya kizazi ya kikoloni'
Feb 13, 2026 22:53Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali uamuzi wa hivi karibuni wa utawala ghasibu wa Israel wa kunyakua ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikisema hatua hiyo inalenga kupanua 'ujenzi wa vitongoji haramu' na kuimarish uvamizi na udhibiti wa masuala ya usalama katika eneo hilo, sambamba na kuendeleza 'mauaji ya kimbari' ya Gaza.
-
Palestina inavyotokomezwa kupitia ukoloni; Iran yalaani uamuzi wa Israel wa kunyakua Ukingo wa Magharibi
Feb 13, 2026 03:51Iran imelaani vikali uamuzi wa hivi karibuni wa utawala wa Israel wa kunyakua ardhi zaidi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ikisema kuwa hatua hiyo inalenga kupanua "ujenzi haramu wa vitongoji vya walowezi za Kizayuni" na kuimarisha ukaliaji mabavu na hatua kali za kiusalama dhidi ya Wapalestina na kuendelea "mauaji ya kimbari" huko Gaza.
-
Hamas yazionya US, Israel: Vita yoyote dhidi ya Iran ni sawa na kushambulia Ulimwengu mzima wa Kiislamu
Feb 12, 2026 07:53Brigedi za al Qassam, tawi ila kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeonya kuwa vita yoyote dhidi ya Iran ni sawa na shambulio dhidi ya Umma mzima wa Kiislamu.
-
Wabangladesh washiriki katika uchaguzi wa kihistoria tangu kuangushwa utawala wa Hasina
Feb 12, 2026 03:00Upigaji kura unaendelea nchini Bangladesh katika uchaguzi unaoonekana kama mtihani muhimu wa kurejea kwa demokrasia nchini humo baada ya vuguvugu la umma lililoongozwa na wanafunzi kumng'oa madarakani kiongozi wa muda mrefu Sheikh Hasina mnamo Agosti 2024.
-
Katika upeo wa unyama, Israel imetumia silaha 'zilizoyeyusha' maelfu ya Wapalestina Ghaza
Feb 11, 2026 23:02Uchunguzi uliofanywa na televisheni ya Al Jazeera ya Qatar umefichua kuwa, utawala wa kizayuni wa Israel umetumia silaha zilizopigwa marufuku kimataifa zenye joto kupindukia katika vita vya mauaji ya kimbari huko Ghaza, na kupelekea "kuyeyuka" maelfu ya miili ya Wapalestina.
-
Hamas: Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu mateka inathibitisha uhalifu wa Israel
Feb 11, 2026 06:02Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kwamba taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ambayo imerekodi ukatili unaofanywa na utawala vamizi wa Israel dhidi ya mateka wa Kipalestina katika vituo na mahabusi zake, inathibitisha zaidi ukiukaji wa sheria za kimataifa ambao haujawahi kutokea unaofanywa na utawala huo.
-
Mpango wa hatua nne wa Netanyahu wa kuumeza Ukingo wa Magharibi
Feb 10, 2026 22:52Uamuzi wa baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu siku ya Jumapili kuhusu Ukingo wa Magharibi ulikuwa msumari wa mwisho katika jeneza la udanganyifu na matumaini ya wale waliofikiri kwamba chini ya kivuli cha makubaliano na wavamizi wa Kizayuni, inawezekana kupata haki za Wapalestina.