-
Mwanamke Afrika Kusini afungwa maisha jela kwa kumuuza binti yake
May 30, 2025 07:32Mwanamke mmoja kutoka Afrika Kusini amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kumuza binti yake mwenye umri wa miaka sita. Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama, mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Joshlin Smith, aliuzwa kwa kiasi cha takribani dola 1,122 za Marekani (sawa na R20,000).
-
Wanawake wa Morocco wadai usawa katika kazi za nyumbani, wataka wanaume nao wavae "aproni" za jikoni
May 02, 2025 07:15Kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, makumi ya wanawake wa Morocco wamefanya maandamano kwenye mitaa ya Casablanca wakisisitiza umuhimu wa kazi za nyumbani zisizo na malipo na kudai usawa wa kijinsia katika kugawana kazi za nyumbani.
-
Jeshi la Msumbiji laokoa wanawake 280 na watoto kutoka mikononi mwa wanamgambo wa Naparama
Apr 26, 2025 11:07Jeshi la Msumbiji limesema kuwa limefanikiwa kuokoa wanawake na watoto wasiopungua 280 waliokuwa wametekwa nyara na wanamgambo wa Naparama katika majimbo ya kaskazini na katikati mwa nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika.
-
Wizi wa kipochi cha Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani wazua kizaazaa
Apr 22, 2025 03:03Ahadi za Donald Trump za kupunguza wizi na uhalifu nchini Marekani si tu ni ahadi chapwa, lakini pia watu wake muhimu ndani ya baraza la mawaziri nao hawajasalimika na wizi na uhalifu.
-
Makumi ya wanawake, watoto wauawa na mabomu ya Wazayuni Gaza
Apr 16, 2025 14:51Mashambulizi makali ya anga ya utawala wa Kizayuni wa Israel yameua shahidi zaidi ya Wapalestina 20, wakiwemo wanawake na watoto wadogo katika Ukanda wa Gaza.
-
Iran: Ufaransa itoe maelezo ya kukamatwa Muirani, mtetezi wa Palestina
Apr 15, 2025 03:15Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa vikali kitendo cha Ufaransa cha kukataa kutoa maelezo ya kukamatwa Mahdieh Esfandiari, raia wa Iran anayeishi katika mji wa Lyon, kaskazini mwa magharibi mwa Ufaransa, zaidi ya mwezi mmoja baada kutiwa kwake mbaroni na vyombo vya usalama vya nchi hiyo ya Ulaya.
-
Wanawake na watoto, wahanga wakuu wa unyanyasaji wa kingono DRC
Apr 12, 2025 06:35Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema katika ripoti yake ya karibuni kabisa iliyotolewa jana Ijumaa kwamba, kwa wastani kila baada ya dakika 30 mtoto mmoja alibakwa wakati wa mapigano makali ya Januari na Februari huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
UN: Mashambulio 36 ya Israel Ghaza kati ya Machi 18 hadi Aprili 9 yameua wanawake na watoto tu
Apr 12, 2025 03:08Umoja wa Mataifa umesema wanawake na watoto wa Kipalestina ndio pekee waliouawa katika mashambulizi yapatayo 36 ya anga yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza tangu katikati ya mwezi Machi na kuonya kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Israel yanahatarisha "kuendelea kuwepo Wapalestina kama jamii".
-
Microsoft yalaaniwa kwa kumfuta kazi mhandisi aliyepinga mauaji ya kimbari Gaza
Apr 10, 2025 07:46Shirika moja la kimataifa limelaani hatua ya kampuni ya Microsoft ya Marekani kumfuta kazi mhandisi wa programu mwenye asili ya Morocco, Ibtihal Aboussad, ambaye aliandamana hadharani kupinga uungwaji mkono wa kampuni hiyo kwa utawala katili wa Israel wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Microsoft.
-
Afrika yashuhudia kupungua vifo vya akina mama na watoto wachanga
Apr 10, 2025 02:55Viwango vya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga barani Afrika vimepungua tangu mwaka 2000, Shirika la Afya Duniani (WHO) limebaini katika ripoti mpya.