Wanawake kumi wahajiri waaga duniai katika bahari ya Mediterania
Jul 01, 2016 03:37 UTC
Wanawake kumi wameaga dunia baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Libya jana Alhamisi.
Habari zinasema kuwa mamia ya wahajiri wengine wamefanikiwa kuokolewa kutoka baharini katika oparesheni mbili za uokoaji. Wanawake hao kumi walikutwa wameaga dunia katika boti ya plastiki. Mlinzi wa pwani ya Italia kwa jina la Kapteni Cosimo Nicastro amesema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuwaokoa wahajiri 107 kutoka katika boti hiyo iliyozama katika bahari ya Mediterania. Wakati huo huo walinzi wa pwani ya Italia wamefanikiwa kuwaokoa wahajiri wengine 116 waliokuwa katika boti nyingine ya plastiki katika eneo hilo hilo palipotokea ajali ya kwanza.