Mamia ya maelfu waandamana barani Ulaya wakitaka kusitishwa vita Gaza
(last modified Mon, 04 Mar 2024 02:29:35 GMT )
Mar 04, 2024 02:29 UTC
  • Mamia ya maelfu waandamana barani Ulaya wakitaka kusitishwa vita Gaza

Mamia ya maelfu ya watu jana waliandamana katika barabara za miji mikuu ya nchi mbalimbali za Ulayakwa wakitaka kusitishwa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza haraka iwezekanavyo; huku idadi ya vifo katika eneo hilo ikipindukia 30,000 kufuatia mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7 mwaka jana.

Wafanya maandamano ambao walikusanyika katika eneo kwa jina la Place de la bastille huko Paris mji mkuu wa Ufaransa huku wakinyeshewa na mvua walisonga mbele kuelekea katika uwanja wa taifa katika kuonyesha mshikamano wao na wananchi madhulumu wa Palestina. 

Wafanya maandamano mjini Paris walikuwa wamebeba bendera za Palestina wakipiga nara na kutoa wito wa kusitishwa vita na mashambuliz ya mabomu ya Israel dhidi ya Gaza. 

Andrea Kallab raia wa Ufaransa mwenye asili ya Lebanon aliyeshiriki katika maandamano hayo alisema kuwa kile kinachotokea katika Ukanda wa Gaza ulio chini ya mzingiro ni jinai dhidi ya binadamu. 

Si Paris pekee iliyoshuhudia maandamano ya kupingavita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza bali huko Berlin Ujerumani pia maelfu ya watu waliandamana katika mji huo mkuu kuonyesha mshikamano kwa wananchi wa Palestina.

Maandamano ya wakazi wa mji wa Berlin Ujerumani kupinga vita vya Gaza 

Wafanya maandamano walikusanyika katika maidani ya Neptune Brunnen wakitaka kukomesha kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina. Waandamanaji aidha walisikika wakipiga nara na shaari kama" Palestine iwe huru, vita visitishwe sasa, na acha mauaji ya kimbari."