Viogozi wa Waislamu Kenya walalamikia safari ya Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10936-viogozi_wa_waislamu_kenya_walalamikia_safari_ya_netanyahu
Viongozi wa Waislamu nchini Kenya wamekosoa vikali uhusiano wa nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na ziara ya hivi karibuni ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo dhalimu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 10, 2016 02:17 UTC

Viongozi wa Waislamu nchini Kenya wamekosoa vikali uhusiano wa nchi yao na utawala wa Kizayuni wa Israel pamoja na ziara ya hivi karibuni ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo dhalimu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Viongozi hao wameonya kuwa, hatua zozote za kuimarisha uhusiano wa kiusalama, kidiplomasia na kiteknolojia na utawala wa Kizayuni una maana ya kuhalalisha jinai zinazofanywa na Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika ardhi na maeneo matakatifu ya Waislamu. Ili kujadili kadhia hiyo na msimamo wa viongozi wa Kiislamu nchini Kenya kuhusu safari ya Netanyahu nchini humo, tumezungumza na Bi. Nazlin Umar Rajput, Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Waislamu (National Muslim Council of Kenya) na ambaye pia ametangaza azma yake ya kuwania urais nchini Kenya mwaka ujao 2017. Kwa kuanza tumemtaka atufahamishe sababu zilizompelekea kumuandikia barua Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo kulalamikia safari ya Netanyahu….