Mar 14, 2024 07:04 UTC
  • Russia: Islamphobia ni aina ya ubaguzi usiyokubalika

Maria Zakharova Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa Moscow inavihesabu vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu (Islamphobia) kuwani aina ya ubaguzi isiyokubalika.

Zakharova alisema jana katika mkutano na vyombo vya habari huko Moscow kwamba Russia inaunga mkono misimamo ya nchi za Kiislamu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuhusu suala hilo. "Tunapinga ubaguzi na unyanyasaji dhidi ya Waislamu kwa misingi ya udini ili kuhakikisha kuwa dini zinakuwa huru kwa kuheshimu si tu mtu binafsi pekee bali pia kuhakikisha kuwa haki za pamoja za waumini zinaheshimiwa. 

Zakharova amesema Russia itaunga mkono rasimu ya azimio la nchi za Kiislamu katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chini ya anwani "Hatua za Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu" katika Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Islamphobia Machi 15 kila mwaka. 

Chuki dhidi ya Uislamu aina ya ubaguzi isiyokubalika 

Azimio hilo linataja suala la kuheshimu dini ya Uislamu kama sehemu ya misingi ya tamaduni na dini mbalimbali na pia kutoa mwanya wa kuanzisha mamlaka kwa Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na aina hii ya chuki dhidi ya dini fulani.  

Russia ni miongoni mwa nchi zilizounga mkono rasimu ya azimio hili. Wiki jana Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia alikosoa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya na kusema kuwa vitendo hivyo vimefikia kiwango kikubwa katika Bunge la Baraza la Ulaya. 

 

Tags