Apr 08, 2024 07:44 UTC
  • Wimbi la kimataifa la kuwaunga mkono watu wa Gaza

Kufanyika Mkutano wa Kimataifa wa Kimbunga cha Al-Aqsa huko Kuala Lumpur, mji mkuu wa Malaysia kwa kuhudhuriwa na makumi ya asasi zisizo za kiserikali, wasomi, wanafikra, mwakilishi maalum wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi kadhaa za Asia, kunaoneysha wimbi kubwa la uungaji mkono wa kimataifa kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Ghaza dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Habib Reza Arzani, Muambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Malaysia, Kongamano la Kimbunga cha  Al-Aqsa: Mwamko wa Kibinadamu limefanyika kwa ushirikiano wa Jumuia ya Kimataifa ya Kukuribisha pamoja Madhehebu ya Kiislamu, Kitengo cha Kiutamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,  Mashirika ya Ushauri ya Jumuia za wananchi za Malaysia, Taasisi za Kiutafiti za Kiislamu na Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Malaysia, na limedhihirisha uungaji mkono mkubwa wa Waislamu wa Malaysia na eneo zima la Kusini mashariki mwa Asia kwa wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina, hasa Gaza. Kuwepo kwa Seyed Ibrahim Seyed Nuh, Mjumbe wa Jumuiya ya Chama cha Palestina katika Bunge la Malaysia, na  Mohammed Azmi Abdul Hamid, Mkuu wa Baraza la Ushauri la Kiislamu la Malaysia katika mkutano huo pia kunaonyesha uungaji mkono wa kiwango cha juu kwa masuala ya Palestina na hasa Gaza katika serikali na bunge la nchi hiyo.

Maandamano ya wananchi wa Malaysia siku ya Quds

Wazungumzaji katika kongamano hilo sambamba na kulaani jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni walitilia mkazo zaidi  nukta kadhaa muhimu ambazo ni kusimamishwa mashambulizi ya kinyama ya Wazayuni dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia wa Palestina hususan wa Gaza na kuondola mzingiro wa ukanda wa Ghaza ili kurahisisha ufikishwaji misaada ya kibinadamu, kuimarisha umoja wa Waislamu duniani kuhusiana na Gaza, kususiwa bidhaa za Israel na kusimamishwa uhusiano wa aina yoyote ile wa kisiasa na Israel.

Ijapokuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikizuia kusimamishwa vita vya Gaza kwa uungaji mkono wao kwa utawala dhalimu wa Kizayuni, lakini mashinikizo ya waliowengi ulimwenguni yamepelekea kutofikiwa malengo ya utawala huo na waungaji mkono wake huko Ghaza.

Ali Zahedi, Mtaalamu wa masuala ya kisiasa anasema kuhusiana na hilo: "Uungaji mkono wa kimataifa kwa watu wa Ghaza umepelekea kufeli utawala wa Kizayuni na kubanwa zaidi utekelezaji wa njama zake na wa waitifaki wake katika uwanja huo.

Siku ya Quds

Vita vya Gaza sio tu kwamba vimeamsha fikra za waliowengi duniani na kuwafanya wamiminike mitaani kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina, bali pia vimeimarisha na kuyapa nguvu mapambano  ya Wapalestina katika kukabiliana na wavamizi.

Wananchi wa Malaysia pamoja na Waislamu na wapenda uhuru kote duniani daima wamekuwa wakionyesha hasira na kuchukizwa kwao na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni kwa kujumuika kwa wengi mbele ya Ubalozi wa Marekani huko Kuala Lumpur.

Kwa kuzingatia kuwa mkutano  wa kimataifa wa Al-Aqsa umefanyika katika mji mkuu wa Malaysia kwa kuhudhuriwa na makumi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, wasomi, wanafikra, wawakilishi maalum wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi kadhaa za Asia kama vile Indonesia, Singapore, Malaysia, Thailand, Pakistan, Yemen na ushiriki wa mashirika ya Kimataifa ni ishara inayoonyesha kuchukizwa walimwengu na uungaji mkono kwa utawala wa Kizayuni, ambao sio tu kwamba hauko tayari kusimamisha vita vya Gaza, bali pia unaendeleza jinai zake hizo ambazo zimepelekea idadi ya mashahidi kuongezeka na kufikia zaidi ya watu elfu 33.

Kwa hivyo, njia pekee ya kudhoofisha siasa za  nchi zinazounga mkono utawala wa Kizayuni na kuulazimisha utawala huo usitishe jinai zake huko Ghaza ni kuimarisha uungaji mkono wa kimataifa na kususiwa bidhaa za utawala hjuo unaoikalia kwa mabavu al Quds Tukufu.

Wakati huo huo, fikra za waliowengi katika nchi ambazo serikali zao zina uhusiano mbalimbali wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi na watawala wa Tel Aviv kwa kuzidisha mashinikizo dhidi ya tawala zao zinaweza kuanda uwanja wa  kushinikizwa zaidi watawala wa Kizayuni. Wazayuni hawakufikiria kwamba wangewahi kukabiliwa na upinzani mkubwa na kulaaniwa kimataifa, jambo ambalo limewapa Wapelastina nguvu ya kuimarisha malengo na mapambano yao dhidi ya Wazayuni.

Tags