Apr 18, 2024 11:43 UTC
  • George Galloway
    George Galloway

Mwanasiasa maarufu wa Uingereza amejibu mashambulizi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akihoji: "Kwa nini hukulaani vikali shambulio la Israel kwenye sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria."

 Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria katika shambulio la kigaidi lililoua shahidi washauri saba waandamizi wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu. 

 Jumatatu, Aprili 1, 2024, utawala wa Kizayuni wa Israel ulishambulia sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria katika shambulio la kigaidi lililoloua shahidi washauri saba waandamizi wa kijeshi wa Jamhuri ya Kiislamu. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Iran, Ayatullah Ali Khamenei alisema baada ya hujuma hiyo ya kigaidi kuwa hatua hiyo ya Tel Aviv ni shambulio dhidi ya ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa utawala wa Kizayuni utaadhibiwa kwa shambulio hilo.

Kuhusiana na suara hilo, Jumapili asubuhi tarehe 14 Aprili 2024, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, liliuadhibu utawala huo jeuri kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drone) na makombora kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika operesheni iliyopewa jina Ahadi ya Kweli.

Katika mkondo huo, mwanasiasa nguli wa Uingereza, George Galloway ambaye alichaguliwa hivi majuzi katika Bunge la nchi hiyo katika uchaguzi mdogo, amemuuliza Waziri Mkuu, Rishi Sunak, kwamba: "Kwa

nini hukulaani utawala wa Israel uliposhambulia sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria?

Akijibu swali la Galloway, Sunak amesema: Hakuna uwiano kati ya hujuma ya Israel katika

ubalozi mdogo wa Iran na mashambulizi ya kulipiza kisiasi ya Iran, na amedai kuwa, sio sahihi kujaribu kufungamanisha hatua hizo mbili. 

Waziri Mkuu wa Uingereza pia amesema katika kikao cha serikali na wabunge kwamba serikali yake haitashiriki katika hatua yoyote ya kijeshi ya Israel dhidi ya Iran, lakini itatoa msaada zaidi wa ulinzi kwa utawala huo haramu.