Maduro ashinda uchaguzi wa rais wa Venezuela kwa muhula wa tatu
(last modified Mon, 29 Jul 2024 06:01:36 GMT )
Jul 29, 2024 06:01 UTC
  • Maduro ashinda uchaguzi wa rais wa Venezuela kwa muhula wa tatu

Nicolás Maduro ameshinda uchaguzi wa rais wa Venezuela na kuchaguliwa kwa muhula wa tatu kuwa rais wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa IRNA, Tume ya Uchaguzi ya Venezuela imetangaza kuwa Maduro ameshinda uchaguzi wa rais wa nchi hiyo kwa kupata 51.2% ya kura.
 
Mkuu wa tume hiyo Elvis Amoroso amesema, Maduro mwenye umri wa miaka 61 amejipatia asilimia 51 ya kura, akimshinda mgombea wa upinzani Edmundo González, ambaye amepata asilimia 44. Ameeleza kuwa matokeo hayo yametokana na matokeo yaliyokusanywa katika asilimia 80 ya vituo vya kupigia kura, hivyo kuashiria mwelekeo wa kutobadilika matokeo yaliyosalia.
Maduro katika kampeni za uchaguzi

Ofisi ya Rais wa Venezuela ilitangaza ushindi wa kiongozi huyo katika uchaguzi wa urais saa chache zilizopita, lakini ikaomba kusubiri kutangazwa kwa matokeo rasmi na Tume ya Uachaguzi ya nchi hiyo.

 
Waangalizi wa uchaguzi kutoka Afrika Kusini wametangaza kuwa mchakato wa upigaji kura katika uchaguzi wa rais wa Venezuela ulikuwa huru, wa haki na wa uwazi.
 
Raia wa Venezuela walipiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais ajaye wa nchi yao.
 
Ushindani mkubwa katika uchaguzi wa mara hii ulikuwa kati ya Nicolas Maduro na Edmundo Gonzalez.../

 

Tags