"Urais pia ni kazi ya watu weusi", Michelle Obama amwambia Trump
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115506-urais_pia_ni_kazi_ya_watu_weusi_michelle_obama_amwambia_trump
Michelle Obama amemshambulia mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Chama cha Democratic uliofanyika jana Jumatano, akikosoa shakhsia yake na mashambulio ya kibaguzi yaliyomlenga yeye na mumewe, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.
(last modified 2024-08-22T03:05:01+00:00 )
Aug 22, 2024 03:05 UTC
  • Michelle Obama
    Michelle Obama

Michelle Obama amemshambulia mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Chama cha Democratic uliofanyika jana Jumatano, akikosoa shakhsia yake na mashambulio ya kibaguzi yaliyomlenga yeye na mumewe, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.

Michelle Obama amesema kuhusu Trump kwamba: "Mwono na mtazamo wake finyu na mdogo kuhusu ulimwengu umemfanya ahisi hatari kutoka kwa watu wawili waliofanikiwa, walioelimika sana ambao pia imesadifu kuwa ni weusi."

Michelle Obama amemdhihaki Donald Trump kwa kuashiria katika kampeni za uchaguzi "nyadhifa zinazoshikwa na watu nyeusi" huko Marekani ambazo anadai zinachukuliwa kutoka kwao na wahamiaji wanaovuka mpaka na kuingia nchini humo.

"Nani atamjuzi Trump kwamba hata kazi anayoitafuta kwa sasa (ya kuingia White House) inaweza kuwa moja ya kazi  Wamarekani weusi?", amesema Michelle Obama huku akishangiliwa na hadhirina. 

Michelle Obama amshambulia Trump kutokana na mitazamo yake ya kibaguzi

Trump alianza maisha yake ya kisiasa kwa mashambulizi yasiyo na msingi na madai ya ubaguzi wa rangi ambayo yalitilia shaka kuzaliwa Barack Obama nchini Marekani na jinsi alivyopata uraia wa Marekani. Vilevile ameanzisha mashambulizi kama hayo dhidi ya mgombea wa sasa wa Chama cha Democratic, Kamala Harris.

Harris anatazamiwa kuchuana na Trump katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Marekani baadaye mwaka huu. 

Harris amekuwa akikabiliwa na mashambulizi ya kibaguzi kutoka kwa Trump, baadhi ya Republican katika Congress na wanaharakati wa mrengo wa kulia.