Madai ya unyanyasaji wa kijinsia yatikisa tasnia ya filamu nchini India
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115802-madai_ya_unyanyasaji_wa_kijinsia_yatikisa_tasnia_ya_filamu_nchini_india
Madai yaliyotolewa juu ya kuweko unyanyasaji wa kijinsia yameitikisa tasnia ya filamu nchini India na kuzua maswali mengi.
(last modified 2026-07-02T04:13:23+00:00 )
Aug 30, 2024 03:49 UTC
  • Madai ya unyanyasaji wa kijinsia yatikisa tasnia ya filamu nchini India

Madai yaliyotolewa juu ya kuweko unyanyasaji wa kijinsia yameitikisa tasnia ya filamu nchini India na kuzua maswali mengi.

Mada ambayo imekuwa ikigonga vichwa vya habari na kutikisa tasnia yenye shughuli nyingi ya filamu katika jimbo la Kerala kusini mwa India tangu wiki iliyopita imekuwa ni madai, maafisa kujiuzulu na malalamiko ya polisi.

Jimbo hilo limekuwa likishuhudia msururu wa madai ya unyanyasaji wa kijinsia kwa baadhi ya nyota wa kiume tangu ripoti ya kihistoria iliyoangazia shida na changamoto zinazowakabili wanawake katika tasnia hiyo kutolewa wiki iliyopita.

Maandamano ya kulalamikia unyanyasaji wa kijinsia katika tasnia ya filamu nchini India

 

Sekta hii, ambayo hutengeneza takribani filamu 150-200 za lugha ya Kimalayalam kwa mwaka, ni biashara muhimu, iliyochangamka ambayo imetengeneza baadhi ya filamu za sinema zenye sifa kuu na zinazoendelea kuibuka kutoka India.

Lakini ripoti hiyo ya kurasa 290 ya jopo la wanachama watatu - inayoitwa kamati ya Hema - ilielezea kwa kina matatizo yanayowakabili wanawake katika sekta ya sinema ya Kimalayalam, ikiwa ni pamoja na mazingira duni ya kazi na unyanyasaji wa kijinsia uliokithiri.

Madai ya ripoti hiyo yameibua maswali mengi kuhusiana na sekta hiyo muhimu ya filamu nchini India hasa kutokana na kuhusisha baadhi ya wacheza filamu na watu mashuhuri.