Watoto wa Uingereza ndio watoto wenye huzuni zaidi barani Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i115804-watoto_wa_uingereza_ndio_watoto_wenye_huzuni_zaidi_barani_ulaya
Imeelezwa kuwa, watoto wa Uingereza ndio watoto wenye ghamu na huzuni zaidi ikilinganishwa na watoto wa mataifa mengine barani Ulaya.
(last modified 2024-08-30T03:50:31+00:00 )
Aug 30, 2024 03:50 UTC
  • Watoto wa Uingereza ndio watoto wenye huzuni zaidi barani Ulaya

Imeelezwa kuwa, watoto wa Uingereza ndio watoto wenye ghamu na huzuni zaidi ikilinganishwa na watoto wa mataifa mengine barani Ulaya.

Taasisi ya Watoto nchini Uingereza imetangaza kwamba, kiwango cha furaha miongoni mwa vijana wa Uingereza wenye umri wa miaka 15, ikilinganishwa na wenzao wa Ulaya, ni cha chini zaidi kuliko katika nchi zote za bara hilo.

Mark Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watoto Nchini Uingereza (The Children's Society) amesema kuwa, kengele ya hatari imeshalia na vijana wa Uingereza wanakabiliwa na hali ya 'mdororo wa furaha'.

Kulingana na tangazo la Jumuiya ya Watoto ya Uingereza, katika uchunguzi wa kulinganisha kiwango cha kuridhika kwa vijana katika nchi 27 za Ulaya, imebainika kuwa nchini Uingereza, 25% ya watoto wa miaka 15 wanaridhika kidogo na maisha yao ambapo kwa mfano, nchini Uholanzi, 7% ya vijana wa umri huu hawajaridhika na maisha yao.

 

Kulingana na ripoti hii, kiwango cha kuridhika kwa vijana wa Uingereza wenye umri wa miaka 15 na maisha kiko chini zaidi kuliko nchi yoyote baranii Ulaya.

Mnamo 2021 na 2022, kiwango cha furaha na kuridhika kwa jumla na maisha ya watoto wa miaka 10-15 nchini Uingereza, pamoja na uhusiano wao na familia, marafiki, shule na kazi za nyumbani, ingawa kilikuwa ni chawastani, ikilinganishwa na 2009 na 2010 lakini kimepungua.

Kulingana na ripoti ya "Taasiisi ya Watoto", kuwa chini hali ya kuridhika na maisha kati ya vijana wa Uingereza ni angalau mara mbili ya kuridhika kwa vijana katika mataifa ya Finland, Denmark, Romania, Ureno, Croatia na Hungary.