Maandamano dhidi ya Israel yafanyika katika nchi mbalimbali
https://parstoday.ir/sw/news/world-i119608-maandamano_dhidi_ya_israel_yafanyika_katika_nchi_mbalimbali
Maelfu ya wafuasi wa wananchi wa Palestina wamefanya maandamano katika miji mingi muhimu duniani ikiwemo Paris, Berlin, Santiago, Amsterdam, Copenhagen, Istanbul, Rome, Manchester na London kulaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Dec 02, 2024 03:37 UTC
  • Maandamano dhidi ya Israel yafanyika katika nchi mbalimbali

Maelfu ya wafuasi wa wananchi wa Palestina wamefanya maandamano katika miji mingi muhimu duniani ikiwemo Paris, Berlin, Santiago, Amsterdam, Copenhagen, Istanbul, Rome, Manchester na London kulaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

Washiriki wa maandamano hayo wametaka kusitishwa undumakuwili na kuuadhibu utawala wa Kizayuni kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi wa Palestina hususan watoto.

Nchini Uhispania maandamano hayo yamefanyika katika miji 50, ukiwemo mji mkuu Madrid, kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina, na waandamanaji hao wametaka kusitishwa vita mara moja katika Ukanda wa Gaza.

Huko London, zaidi ya waandamanaji 125,000 walitangaza mshikamano wao na watu wa Palestina na Gaza.

Washiriki wa maandamano hayo waliikosoa serikali ya Uingereza kwa kuunga mkono utawala wa Kizayuni na kusisitiza juu ya kuchukua msimamo madhubuti wa kuhitimisha vita katika Ukanda wa Gaza.

Huko Berlin, mji mkuu wa Ujerumani na miji mingine 10 ya nchi hiyo, washiriki wa maandamano dhidi ya Israel waliobeba bendera ya Palestina na mabango yanayoonyesha mshikamano na taifa la Palestina wamelaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na Lebanon.