Russia: BRICS kuanzisha mfumo wa malipo wa 'dijitali' kwa wanachama
Waziri wa Fedha wa Russia amesema kuwa nchi wanachama wa kundi la BRICS zinachunguza hatua kadhaa za ubunifu wa kifedha ikiwemo kuanzisha mfumo wa malipo wa kidijitali ili kutoa huduma za kifedha ndani ya kambi hiyo ya kiuchumi.
Anton Siluanov amesema kuwa wamejikita katika kuzingatia ubunifu mbalimbali wa kifedha katika kalibu ya kundi la BRICS, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo wa kuvuka mipaka utakaoshirikisha ushirikiano wa pande mbili katika sarafu za taifa kwa kuzingatia teknolojia ya kidijitali na rasilimali fedha.
Wanachama wa sasa wa kundi la BRICS ni Brazil, Russia, India, China , Afrika Kusini, Misri, Iran, UAE, Saudi Arabia, Indonesia na Ethiopia.
Baadhi ya nchi zinazoendelea kama Algeria, Belarus, Bolovia, Cuna, Indonesia, Kazakhstan, Malaysia, Nigeria, Thailand, Uturuki, Uganda, Uzbekistan na Vietnam zimeeleza nia na hamu yao ya kujiunga na kundi hilo lialoibukia kiuchumi.
Waziri wa Fedha wa Russia amesema, "kuanzisha miundombinu ya kifedha ni muhimu sana kwa maendeleo ya biashara na uchumi wa nchi zetu."
Katika hatua yake ya kuizuia BRICS kuachana na matumizi ya sarafu ya dola, Rais Donald Trump wa Marekani amezitishia nchi wanachama wa kundi hilo dhidi ya hatua yoyote ya kudhoofisha sarafu ya dola.