Wahka watanda Marekani kwa hofu ya mashambulizi ya mtandaoni ya Iran
(last modified Tue, 01 Jul 2025 02:33:44 GMT )
Jul 01, 2025 02:33 UTC
  • Wahka watanda Marekani kwa hofu ya mashambulizi ya mtandaoni ya Iran

Vyombo vya serikali ya Marekani vimetahadharisha kuhusu uwezekano wa kuendelea mashambulizi ya mtandaoni ya Iran dhidi ya miundombinu na mitandao ya nchi hiyo hususan makampuni yenye mfungamano na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mtandao wa ABC, umenukuu vyombo vya serikali ya Marekani, vikionya kwamba makundi ya mtandaoni yenye uhusiano na Iran na wadukuzi huenda wakaendelea na shughuli zao za kulenga vifaa na mitandao ya Marekani.

Mtandao huo wa Marekani umeendelea kuwa makampuni ya sekta ya ulinzi, hasa yale yenye uhusiano na Israel, yanakabiliwa na hatari inayoongezeka kila siku.

Awali Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani ilikuwa imeonya kwamba uwezekano wa mashambulizi ya mtandaoni ya wadukuzi wa Iran umeongezeka zaidi kutokana na mvutano kati ya Iran, Marekani na Israel.

Vyombo vya habari pia vimetangaza kuwa katika siku za hivi karibuni, benki za Kimarekani, wakandarasi wa masuala ya ulinzi na makampuni ya mafuta nchini humo yamekuwa yakilengwa kwa mashambulizi ya mtandaoni yanayohusishwa na Iran.