Vijana wa Ulaya hawana imani na demokrasia ya Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i127942-vijana_wa_ulaya_hawana_imani_na_demokrasia_ya_magharibi
Uchunguzi wa maoni uliofanywa katika nchi za Ulaya umenyesha kuwa nusu tu ya vijana wa Ufaransa na Uhispania tu ndio wamesema wanaamini kuwa demokrasia ndiyo njia bora ya utawala.
(last modified 2025-07-05T04:13:48+00:00 )
Jul 05, 2025 04:13 UTC
  • Vijana wa Ulaya hawana imani na demokrasia ya Magharibi

Uchunguzi wa maoni uliofanywa katika nchi za Ulaya umenyesha kuwa nusu tu ya vijana wa Ufaransa na Uhispania tu ndio wamesema wanaamini kuwa demokrasia ndiyo njia bora ya utawala.

Tovuti ya gazeti la The Guardian imeeleza kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na Chuo Kikuu Huria cha Berlin nchini Ujerumani, asilimia 57 ya kizazi kipya cha Ulaya, kinachojulikana kama Generation Z, wanapendelea demokrasia kuliko aina nyingine za serikali.

Gazeti hilo limeandika kuwa: Kwa mujibu wa matokeao ya uchunguzi huo wa maoni, kiwango cha watu kuvutiwa na demokrasia katika nchi za Ulaya kinatofautiana kutoka nchi hadi nchi. Kwa mfano, huko Poland ni asilimia 48 tu, nchini Uhispania na Ufaransa karibu asilimia 51-52 wameonyesha kuvutiwa na utawala wa demokrasia, huku Ujerumani, asilimia 71 yya vijana wakifadhilisha demokrasia. 

Kwa mujibu wa gazeti hilo, takriban moja ya kumi ya vijana wa Ulaya walisema hawajali hata kidogo ikiwa serikali yao ni ya kidemokrasia au la. Katika uchunguzi huo, asilimia 14 ya vijana wa Ulaya wamesema kuwa hawajui lolote kuhusu demokrasia au hahwajytoa jibu kuhusu suala hilo.