Takwimu za kutisha kuhusu hali ya umaskini barani Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/world-i128602-takwimu_za_kutisha_kuhusu_hali_ya_umaskini_barani_ulaya
Licha ya sura yake ya kumetameta kama kimbilio la ufanisi na hali bora, takwimu zenye kushtua zinaonyesha kwamba Ulaya inaficha hali tete na ya kutisha ya kijamii. Takwimu zinaonyesha kuwa, umaskini unaenea katika vitovu vya miji mikubwa na vitongoji vilivyosahaulika vya miji ya Ulaya, na nafasi ambazo hapo awali zilitoa utulivu kwa tabaka la kati zinazidi kupungua.
(last modified 2025-09-22T12:23:50+00:00 )
Jul 22, 2025 04:32 UTC
  • Takwimu za kutisha kuhusu hali ya umaskini barani Ulaya

Licha ya sura yake ya kumetameta kama kimbilio la ufanisi na hali bora, takwimu zenye kushtua zinaonyesha kwamba Ulaya inaficha hali tete na ya kutisha ya kijamii. Takwimu zinaonyesha kuwa, umaskini unaenea katika vitovu vya miji mikubwa na vitongoji vilivyosahaulika vya miji ya Ulaya, na nafasi ambazo hapo awali zilitoa utulivu kwa tabaka la kati zinazidi kupungua.

Sambamba na kupungua nafasi ya serikali katika masuala ya kijamii na kupanda kwa gharama za maisha, mamilioni ya watu wa Ulaya wanajikuta wamenaswa kati ya ukosefu wa ajira na tatizo la makazi. 

Data rasmi zinaonyesha ukweli tofauti kuhusu Bara Ulaya. Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na jukwaa la All Europe mnamo Julai 2024, takriban 20% ya wakazi wa Umoja wa Ulaya—sawa na mtu 1 kati ya kila 5— wako katika hatari ya umaskini au kutengwa na jamii.

Ripoti iliyotolewa na Statista, kampuni ya Ujerumani iliyobobea katika masuala ya soko na data ya watumiaji, zinaonyesha kuwa takriban watu milioni 100 katika Umoja wa Ulaya wako katika hatari ya umaskini au kutengwa na jamii, wakiwakilisha takriban moja ya tano ya watu wa bara hilo.

Kijana ombaomba kwenye barabara ya waenda kwa miguu huko Dortmund, Ujerumani.

Asilimia hii ya kushangaza inajumuisha mamilioni ya watu wanaoishi kando ya jamii za Ulaya, chini ya kivuli cha mifumo ya usaidizi wa kijamii inayoshindwa kudhibiti ukosefu wa usawa unaokua siku baada ya siku.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa, umaskini barani Ulaya una aina nyingi na tofauti. Umaskini katika bara hilo, mara zote hauna maana ya njaa au ukosefu wa makazi pekee. Badala yake, mara nyingi hudhihirika katika kushindwa kukidhi gharama za kimsingi za maisha kama vile makazi, nishati kama umeme na gesi, elimu na hata huduma ya afya.

Data zinaonyesha kwamba karibu 10% ya wafanyakazi katika Umoja wa Ulaya wanaishi chini ya mstari wa umaskini, suala linalodhoofisha imani ya jadi kwamba kazi hutoa kinga ya moja kwa moja dhidi ya umaskini.