Chama cha Kinazi Marekani: Trump ni 'fursa halisi'
https://parstoday.ir/sw/news/world-i12871-chama_cha_kinazi_marekani_trump_ni_'fursa_halisi'
Kiongozi mmoja wa chama cha Kinazi nchini Marekani amesema kuwepo Donald Trump, mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya chama cha Republicans ni "fursa halisi" katika uchaguzi huo kwa waungaji mkono wa fikra ya ubora wa kizazi cha watu weupe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 08, 2016 10:13 UTC
  • Chama cha Kinazi Marekani: Trump ni 'fursa halisi'

Kiongozi mmoja wa chama cha Kinazi nchini Marekani amesema kuwepo Donald Trump, mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya chama cha Republicans ni "fursa halisi" katika uchaguzi huo kwa waungaji mkono wa fikra ya ubora wa kizazi cha watu weupe.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, Rocky Suhayda, mwenyekiti wa chama cha kibaguzi cha Kinazi alitoa matamshi hayo katika kipindi maalumu cha redio kilichorekodiwa mwezi uliopita.

Rocky Suhayda, kiongozi wa chama cha Kinazi cha Marekani

Akizungumza katika kipindi hicho, Suhayda alisema:"Endapo Trump atashinda itakuwa fursa halisi kwa watu kama wazungu wenye misimamo ya utaifa ili kuitumia kwa busara fursa hiyo kwa ajili ya kuunda chama kama cha watu weusi ndani ya Kongresi".

Chama cha Kinazi cha Marekani kiliundwa mwaka 1959, na makao makuu yake yako katika jimbo la Virginia.

Chama cha Nazi cha Marekani

Mbali na Rocky Suhayda, Rachel Pendergraft, mratibu taifa wa chama cha Mashujaa ambacho ni mbeba bendera ya kundi la kibaguzi la Ku Klux Klan linalounga mkono ubora wa kizazi cha watu weupe, amesema kumuunga mkono Trump  kutafungua njia ya kuanzisha awamu mpya ya mazungumzo kwa lengo la kuvutia wanachama wapya katika chama hicho.

Kabla ya hapo, David Duke, kiongozi wa zamani wa kundi la Ku Klux Klan, naye pia alitangaza uungaji mkono wake kwa Donald Trump.

Trump akinasibishwa na Manazi

Hata hivyo alipohojiwa na kanali ya televisheni ya CNN mapema mwezi Februari kuhusiana na kundi hilo la kibaguzi linalotetea ubora wa kizazi cha watu weupe,Trump alidai kuwa hajui chochote kuhusiana na kundi hilo.../