Putin: Tumefikia 'maelewano' na Trump kumaliza vita vya Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i130286-putin_tumefikia_'maelewano'_na_trump_kumaliza_vita_vya_ukraine
Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kuwa, alifikia "maelewano" na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpamgo wa kumaliza vita vya Ukraine, katika mkutano wao huko Alaska mwezi uliopita.
(last modified 2025-09-01T08:25:43+00:00 )
Sep 01, 2025 08:25 UTC
  • Putin: Tumefikia 'maelewano' na Trump kumaliza vita vya Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kuwa, alifikia "maelewano" na Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mpamgo wa kumaliza vita vya Ukraine, katika mkutano wao huko Alaska mwezi uliopita.

Lakini hakusema kama atakubali mazungumzo ya amani na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky yaliyosimamiwa na Trump, ambaye inaonekana aliitaja Jumatatu kama tarehe ya mwisho ya jibu la Putin.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kilele nchini China, Putin aliendelea kutetea uamuzi wake wa kuivamia Ukraine, kwa mara nyingine tena akilaumu vita vya nchi za Magharibi.

Kufuatia mkutano wa Alaska, mjumbe maalum wa Marekani Steve Witkoff alisema Putin amekubali kudhaminiwa usalama wa Ukraine kama sehemu ya uwezekano wa makubaliano ya amani ya siku zijazo, ingawa Moscow bado haijathibitisha hilo.

Putin alikuwa akizungumza mjini Tianjin katika mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano la Shanghai, ambapo alikutana na Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Aidha Putin aliwashukuru viongozi wa China na India kwa msaada wao na juhudi zao za "kuwezesha utatuzi wa mgogoro wa Ukraine".

China na India ndio wanunuzi wakubwa wa mafuta ghafi ya Russia, na yamekuwa yakikosolewa na mataifa ya Magharibi kwa kuunga mkono uchumi wa Moscow ambao umeathiriwa na juhudi za vita.

Katika hotuba yake, Putin pia alisema kwamba "maelewano yaliyofikiwa" katika mkutano wake na Trump huko Alaska ni "hatua moja mbele, kuelekea njia ya amani nchini Ukraine".