Waziri Mkuu mpya wa Ufaransa Sebastien Lecornu ajiuzulu
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amekubali kujiuzulu Waziri Mkuu aliyemteua hivi karibuni baada ya kukosolewa kuhusu safu ya baraza lake la mawaziri.
Waziri Mkuu wa Ufaransa Sebastien Lecornu amejiuzulu wiki chache baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo hatua iliyozidisha mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Ofisi ya Rais wa Ufaransa imetangaza katika taarifa yake hii leo kwamba Rais Emmanuel Macron amekubali kujiuzulu kwa muitifaki wake huyo wa karibu.
Jana Jumapili Lecornu alitangaza baraza lake la mawaziri yaani muda wa karibu mwezi mmoja tangu ateuliwe kuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa.
Baraza la mawaziri lilikuwa limepanga kufanya mkutano wake wa kwanza leo alasiri, lakini safu ya mawaziri awaliokuwa wameteuliwa na Sabastien Lecornu iliwakasirisha wapinzani na pia waitifaki.
Lecornu, waziri wa zamani wa ulinzi, ni waziri mkuu wa tano kuwahi kuteuliwa na Macron katika kipindi cha miaka miwili.
Lecornu ambaye aliteuliwa na Rais Macron katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja uliopita baada ya kusambaratika kwa baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Francois Bayrou jana Jumapili aliwaslisisha safu ya Baraza lale la Mawaziri ambalo wachambuzi wa mambo wanasema kuwa halina mabadiliko makubwa.
Wapiga kura nchini Ufaransa kwa muda sasa wamekuwa wakitaka kufanyika mabadiliko katika safu ya baraza la mawaziri.
Kiongozi wa chama cha Kijani nchini Ufaransa Marime Tondelier amesema kuwa waitifaki wa Rais Macron walikuwa wameidhalilisha Ufaransa kidemokrasia huku Msoshalisti Boris Vallad akiituhumu serikali kwa kuitumbukiza Ufaransa katika machafuko kila uchao.