Araqchi na Lavrov wafanya mashauriano ya simu kuhusu Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133108-araqchi_na_lavrov_wafanya_mashauriano_ya_simu_kuhusu_gaza
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wa pande mbili.
(last modified 2025-11-12T23:09:22+00:00 )
Nov 12, 2025 23:09 UTC
  • Sergei Lavrov na Seyyed Abbas Araqchi, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia na Iran
    Sergei Lavrov na Seyyed Abbas Araqchi, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia na Iran

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wa pande mbili.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetangaza kuwa, Sergei Lavrov na Seyyed Abbas Araqchi, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Russia na Iran wamejadili na kubadilishana mawazo kwa njia ya simu kuhusu masuala ya pande mbili na masuala ya kieneo ikiwemo Gaza.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa Araqchi na Lavrov wamekaribisha kwa mikono miwili makubaliano yaliyofikiwa kati ya Afghanistan na Pakistan kuhhuusiana na kusitisha mapigano katika eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Russia pia wamejadili kuhusu matukio ya Asia Magharibi hususan Gaza na kuchunguzwa suala hili katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na hali katika Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.

Mawaziri hao wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na Jamhuri ya Kiislamuu ya Iran wamesisitiza tena kujitolea kwao kwa utekelezaji usio na masharti wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kikakati Kamili kati ya Rusiana Iran, ambao ulianza kutekelezwa tarehe 2 Oktoba.