Waziri Mkuu mpya wa Hungary: Netanyahu atakamatwa kama ataingia nchini
-
Péter Magyar
Péter Magyar Waziri Mkuu mpya wa Hungary, amesema kuwa iwapo Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel ataingia nchini humo, atakamatwa kwa kesi ya uhalifu wa kivita.
Waziri Mkuu mteule wa Hungary, ameashiria nia ya serikali ya Waziri Mkuu wa sasa, Viktor Orbán ya kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) na kusema: "Nimemweleza wazi Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kwamba msimamo wetu madhubuti ni kwamba tutasimamisha mchakato wa kujiondoa kwenye Mahakamani ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), na Hungary itabaki kuwa mwanachama katika mahakama hiyo."
Ameongeza kuwa: "Kama nchi ni mwanachama wa ICC na mtu anayetafutwa na mahakama hiyo ataingia katika ardhi yetu, mtu huyo anatakiwa kukamatwa."
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yenye makao yake mjini The Hague nchini Uholanzi Alhamisi, Novemba 22, 2024, ilitoa amri ya kukatakwa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wake wa vita Yoav Gallant kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya binadamu na kutumia njaa kama silaha dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.
Kwa upande mwingine, Afrika Kusini mnamo Desemba 2023 iliwasilisha malalamiko dhidi ya utawala katili wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ikisema kuwa utawala huo umevunja Mkataba wa Kuzuia Mauaji ya Kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Israel imeua karibu Wapalestina elfu 75 katika mauaji ya kimbari ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.