Bennett: Clinton na mumewe wametajirika kwa pesa za Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i18694-bennett_clinton_na_mumewe_wametajirika_kwa_pesa_za_saudia
Ofisa wa zamani wa jeshi la Marekani na mchambuzi wa siasa amesema mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat Hillary Clinton na mumewe wake Bill Clinton wamechuma utajiri wao kutokana na kuiuzia Saudi Arabia ushawishi wa serikali ya Washington.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 03, 2016 03:53 UTC
  • Bennett: Clinton na mumewe wametajirika kwa pesa za Saudia

Ofisa wa zamani wa jeshi la Marekani na mchambuzi wa siasa amesema mgombea wa urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrat Hillary Clinton na mumewe wake Bill Clinton wamechuma utajiri wao kutokana na kuiuzia Saudi Arabia ushawishi wa serikali ya Washington.

Bennett ambaye aliwahi kuwa ofisa mkuu wa kitengo cha vita vya kisaikolojia cha jeshi la Marekani amesema Clinton na mumewe wamepata utajiri na ushawishi mkubwa katika siasa za Marekani kwa kunadi ushawishi wa serikali ya Washington kwa Saudia na washirika wake katika eneo kama vile Morocco, Qatar na Kuwait.

Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton

Mchambuzi huyo wa siasa za Marekani amesema Wakfu wa Clinton umekuwa ukipokea mamilioni ya dola kupitia Benki ya Union ya Uswisi ili kueneza Uwahabi wa Saudia kwa njia zisizo za moja kwa moja katika eneo la Mashariki ya Kati.

Bennett amesema Wakfu wa Clinton ulianza kupokea fedha hizo kutoka Saudia na washirika wake wakati Hillary Clinton alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kati ya mwaka 2009 na 2013.

Hii ni katika hali ambayo, Polisi ya Upelelezi Marekani FBI imetoa nyaraka za kurasa 129, zilizofichua namna Bill Clinton katika siku za mwisho ofisini alivyotoa msamaha kwa mfanyabiashara mtoro, Marc Rich, aliyekuwa akikabiliwa na kashfa nyingi za ufisadi. Rich ambaye alikimbilia nchini Uswisi mwaka 1983, anakabiliwa na tuhuma za ufisadi wa kifedha na kukwepa kulipa kodi.