Umoja wa Ulaya warefusha vikwazo dhidi ya Russia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i21754-umoja_wa_ulaya_warefusha_vikwazo_dhidi_ya_russia
Umoja wa Ulaya umeongeza muda wa vikwazo dhidi ya Russia.
(last modified 2026-04-24T06:29:55+00:00 )
Dec 19, 2016 23:35 UTC
  • Umoja wa Ulaya warefusha vikwazo dhidi ya Russia

Umoja wa Ulaya umeongeza muda wa vikwazo dhidi ya Russia.

Baraza la Umoja wa Ulaya limebainisha katika taarifa yake liliyoitoa jana Jumatatu kuwa vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Russia ili kulenga sekta maalumu za kiuchumi za nchi hiyo vimeongezwa muda hadi kufikia tarehe 31 mwezi Julai mwaka kesho. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vikwazo hivyo vimezilenga hasa taasisi tano mashuhuri za kifedha za Russia pamoja na makampuni tanzu yenye mfungamano na taasisi hizo nje ya Umoja wa Ulaya.

Akitoa radiamali kwa vikwazo hivyo, Vladimir Chizhov Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Ulaya amesema kuwa Brussels haina irada ya kisiasa ya kuiondolea Russia vikwazo hivyo. Itakumbukwa kuwa Umoja wa Ulaya uliiwekea Russia vikwazo baada ya kushadidi mgogoro wa Ukraine. Russia pia imejibu hatua ya Umoja wa Ulaya kwa kuuwekea  vikwazo.

Balozi Vladimir Chizhov, Mwakilishi wa Russia katika EU