Umoja wa Mataifa: Hatua ya Trump inakiuka sheria za kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i24483-umoja_wa_mataifa_hatua_ya_trump_inakiuka_sheria_za_kimataifa
Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, amri iliyotiwa saini na Rais Donald Trump wa Marekani ya kuzuia raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini Marekani ni kinyume cha sheria za kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 31, 2017 00:39 UTC
  • Umoja wa Mataifa: Hatua ya Trump inakiuka sheria za kimataifa

Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, amri iliyotiwa saini na Rais Donald Trump wa Marekani ya kuzuia raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia nchini Marekani ni kinyume cha sheria za kimataifa.

Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Zeid al-Hussein amesema kuwa ni marufuku na kinyume cha sheria kuwabagua watu kwa mujibu wa utaifa wao.

Ra’ad al-Hussein ameongeza kuwa, sheria ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini Marekani iliyoanza kutekelezwa Marekani ni ya kikatili na sababu ya kuharibiwa rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya kupambana ipasavyo na ugaidi. 

Image Caption

Msimamo huo wa Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa umetangazwa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kusaini amri inayowazuia raia wa nchi kadhaa za Kiislamu kuingia nchini humo.

Trump akisaini amri ya kuzuia Waislamu kuingia Marekani 

Hatua hiyo ya Trump anayejulikana kwa fikra na misimamo yake ya kibaguzi hususan dhidi ya Waislamu na wahamiaji, imekosolewa sana na nchi na jumuiya mbalimbali za kimataifa za kutetea haki za binadamu. 

Wamarekani waandamana kupinga amri ya Trump