UN yatoa azimio la kuwatetea Waislamu wa Rohingya, Myanmar
https://parstoday.ir/sw/news/world-i26800-un_yatoa_azimio_la_kuwatetea_waislamu_wa_rohingya_myanmar
Nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa zipasisha azimio na kutaka kufunguliwa mshtaka, kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa wale wote wanaohusika na mauaji na kuwatesa Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Mar 24, 2017 11:20 UTC
  • UN yatoa azimio la kuwatetea Waislamu wa Rohingya, Myanmar

Nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa zipasisha azimio na kutaka kufunguliwa mshtaka, kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa wale wote wanaohusika na mauaji na kuwatesa Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.

Nchi 47 wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa zimepiga kura zikiunga mkono rasimu iliyowasilishwa na Umoja wa Ulaya kulaani mateso na mauaji dhidi ya Waislamu wa Rohingya huko Myanmar na kutaka kuchunguzwa suala hilo. Azimio hilo limesisitiza pia ulazima wa kutumwa ujumbe wa uchunguzi huko Myanmar ambao utachunguza vitendo vya unyanyasaji na bughudha wanayokabiliana nayo Waislamu wa kabila la Rohingya yakiwemo mauaji na kuteswa. 

Mkoa wa Rakhine huko kaskazini magharibi mwa Myanmar ni makazi ya Waislamu wa Rohingya zaidi ya milioni moja na tangu mwaka 2012 hadi sasa eneo hilo limekuwa likishuhudia ghasia na vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu. Serikali ya Myanmar pia inajizuia kuwapatia Waislamu hao haki zao za kiraia.

Waislamu wa Rohingya wakielekea mazikoni kumzika mwenzao aliyeuliwa na Mabudha 

Hadi kufikia sasa mamia ya Waislamu wa Rohingya wameuliwa na makumi ya maelfu ya wengine wamezikimbia nyumba zao kwa kuhofia kupoteza maisha na badala yake wamekimbilia katika nchi jirani. Waislamu wa Rohingya karibu elfu 75 wamekimbilia nchini Bangladesh. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Waislamu hao wa Myanmar ni jamii iliyodhulumika zaidi duniani na wamekuwa wahanga wa mateso na unyanyasaji mkubwa.

Wakati huo huo Yanghee Le, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za binadamu huko Myanmar ametaka iundwe kamati ya uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za Waislamu wa Rohingya nchini humo. 

Yanghee Le, Ripota Maalumu wa UN kuhusu Haki za binadamu huko Myanmar