Apr 01, 2017 15:54 UTC
  • UNSC yalaani mashambulizi ya makundi ya Daesh (ISIS) na Boko Haram

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Boko Haram na Daesh (ISIS) katika eneo la Ziwa Chad, barani Afrika.

Baraza hilo limepitisha mpango uliowasilishwa na Uingereza wa kulaani mauaji na ukiukaji wa haki za binaadamu zikiwemo za wanawake na watoto unaofanywa na wanachama wa makundi ya ukufurishaji ya Daesh na Boko Haram.

Sehemu ya mashambulizi ya kundi la Boko Haram

Kadhalika baraza hilo limelaani jinai nyingine za makundi hayo ikiwemo kupora mali, ukatili wa kijinsia, kuwatumia watoto kijeshi kwa lazima sambamba na kuwatumia katika utekelezaji mashambulizi ya kigaidi. Nchi za eneo la Ziwa Chad ikiwemo Cameroon, Chad, Niger na Nigeria zinakabiliwa na mgogoro wa kibinaadamu ambapo hadi sasa mamilioni ya watu wanaoishi kando na ziwa hilo wanaishi katika hali ngumu inayotokana na kuendelea mapigano ya makundi ya wabeba silaha katika eneo.

Namna ambavyo makundi hayo ya Kiwahabi yanavyowatumia watoto wadogo katika jinai

Katika fremu hiyo, duru za habari zimeripoti kwamba Alkhamisi iliyopita, wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haramu waliteka nyara wasichana na wanawake wasiopungua 22 katika shambulizi dhidi ya kijiji cha Bulka, kilichoko karibu na mpaka na Cameroon. Itakumbukwa kuwa, mwaka 2014 kundi hilo la Boko Haram liliteka nyara wanafunzi 276 wa kike waliokuwa wakisoma katika shule ya Chibok, jimbo la Borno, Kaskazini mwa Nigeria. Baadhi yao wasichana hao walibahatika kutoroka na wengine kukombolewa lakini hatima ya kundi kubwa la wasichana hawa bado haijulikani hadi leo hii. 

Sehemu ya jinai za wanachama wa kundi la Daesh dhidi ya raia wa kawaida

 

Tags