Russia yasisitiza kuundwa muungano wa kimataifa wa kutegua mabomu huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/world-i28292-russia_yasisitiza_kuundwa_muungano_wa_kimataifa_wa_kutegua_mabomu_huko_syria
Russia imetaka kuundwa muungano wa kimataifa kwa ajili ya kutegua mabomu ya kutegwa ardhini huko Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 26, 2017 08:46 UTC
  • Russia yasisitiza kuundwa muungano wa kimataifa wa kutegua mabomu huko Syria

Russia imetaka kuundwa muungano wa kimataifa kwa ajili ya kutegua mabomu ya kutegwa ardhini huko Syria.

Sergei Shoigu amependekeza leo katika Kikao cha Sita cha Usalama wa Kimataifa cha kila mwaka huko Mocsow kuwa muungano wa kimataifa unapasa kuundwa ili kushiriki katika oparesheni za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini huko Syria. Waziri wa Ulinzi wa Russia amesema kuwa kuna udharura wa kuanzisha mfuko wa fedha ili kuyalipa mashirika yenye ujuzi yatakayoshiriki katika oparesheni ya kutegua mabomu hayo.

Russia imekuwa ikishiriki pakubwa katika shughuli ya kutegua mabomu ya ardhini huko Syria. Hivi sasa pia kumeasisiwa tawi la kituo cha kimataifa cha Russia kinachoshughulika na uteguaji mabomu huko katika mkoa wa Homs. Aidha wataalamu na wahandisi wa kutegua mabomu wa Russia hivi sasa wanatekeleza oparesheni ya kutegua mabomu yaliyotegwa chini ya ardhi katika miji ya Halab na Tadmir nchini Syria.

Mtaalamu wa kutegua mabomu ya kutegwa ardhini wa Russia akiwa kazini Syria 

Syria ilitumbukia katika hali ya mgogoro tangu mwaka 2011 kufuatia kutekelezwa hujuma kubwa na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono kifedha na kisilaha na Saudia, Marekani na waitifaki wao katika eneo la Mashariki ya Kati kwa lengo la kuiondoa madarakani serikali halali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Bashar al Assad.