Uturuki kuendelea kulisaidia genge la kigaidi la Jab'hatu Nusra
https://parstoday.ir/sw/news/world-i29876-uturuki_kuendelea_kulisaidia_genge_la_kigaidi_la_jab'hatu_nusra
Serikali ya Uturuki imelipa matumaini kundi la kigaidi na ukufurishaji la Jab'hatu Nusra linalotekeleza mauaji na jinai nchini Syria kuwa, itaendelea kuliunga mkono na kulisaidia kwa hali na mali.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2017 23:52 UTC
  • Uturuki kuendelea kulisaidia genge la kigaidi la Jab'hatu Nusra

Serikali ya Uturuki imelipa matumaini kundi la kigaidi na ukufurishaji la Jab'hatu Nusra linalotekeleza mauaji na jinai nchini Syria kuwa, itaendelea kuliunga mkono na kulisaidia kwa hali na mali.

Gazeti la al-Watan limezinukuu duru za upinzani nchini Syria na pia viongozi wa ngazi ya juu wa makundi ya wabeba silaha hususan Jab'hatu Nusra, wakisema kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwepo vikao tofauti baina ya viongozi wa ngazi ya juu wa Uturuki hususan wawakilishi wa idara ya intelijensia na jeshi pamoja na makamanda wa genge hilo la kigaidi ambalo ni sehemu ya muungano wa kigaidi unaoitwa 'Tahriru sh-Sham.' Kwa mujibu wa ripoti hii, katika vikao hivyo wawakilishi wa Uturuki wamewapa matumaini viongozi hao wa kigaidi kwamba serikali ya Ankara itaendelea kuwaunga mkono kwa kuwapatia misaada mbalimbali.

Wanachama wa kundi la  Jab'hatu Nusra

Kadhalika gazeti la al-Watan limesisitiza kuwa, harakati za kundi hilo la kigaidi katika kupata misaada kutoka Uturuki, zilikuja baada ya kushadidi mashinikizo dhidi ya serikali ya Ankara yakiitaka serikali hiyo kufungamana na mpango wa maeneo yaliyopunguzwa migogoro ya Syria na pia mazungumzo ya Marekani na Russia kwa ajili ya kulitokomeza kundi hilo ambalo ni tawi la kundi la al-Qaidah nchini Syria. Aidha gazeti hilo limemnukuu kiongozi mmoja wa Jab'hatu Nusra ambaye alishiriki moja ya vikao hivyo vilivyofanyika katika mji wa al-Raihaniyah nchini Uturuki akisema kuwa, Ankara inautambua uepo wa kundi la Jab'hatu Nusra katika eneo kuwa ni wenye maslahi kwake na kwamba kundi hilo sio sawa na genge la Daesh ambalo kuamiliana nalo kunasababisha hatari. Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya Uturuki kutoa uungaji mkono na misaada kwa magenge ya kigaidi yanayotekeleza mauaji na jinai nchini Syria na Iraq.