WHO: Asilimia 60 ya watu duniani hawapati maji safi na salama
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, asilimia 60 ya watu duniani hawapati maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani imezitaka nchi wanachama kufanya jitihada zaidi kwa ajili ya kudhamini maji safi na salama kwa raia wao kama haja ya awali ya kiumbe mwanadamu kote duniani.
Ripoti hiyo ya WHO imeongeza kuwa, huduma ya kupata maji safi na salama haipasi kuwa kwa ajili ya sehemu ya jamii ya dunia ambayo ina uwezo wa kifedha au kwa ajili ya watu wanaoishi maeneo ya mjini pekee.
Shirika la Afya Duniani limesisitiza katika ripoti hiyo kwamba, uchunguzi umebaini kuwa, asilimia 15 ya wakazi wa nchi za kusini mwa Afrika na karibu asilimia 76 ya watu wa nchi za magharibi mwa Asia na kaskazini mwa Afrika hawapati huduma za fya.