UN: Wakimbizi Waislamu wa Rohingya wanakabiliwa na hatari kubwa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36525-un_wakimbizi_waislamu_wa_rohingya_wanakabiliwa_na_hatari_kubwa
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa una wasiwasi kuhusu hatari zinazowakabili Waislamu wakimbizi wa Rohingya katika wimbi la kufukuzwa huko Myanmar.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 19, 2017 12:55 UTC
  • UN: Wakimbizi Waislamu wa Rohingya wanakabiliwa na hatari kubwa

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa una wasiwasi kuhusu hatari zinazowakabili Waislamu wakimbizi wa Rohingya katika wimbi la kufukuzwa huko Myanmar.

Msemaji wa Kamisheni Kuu ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa (UNHCR), William Spindler amesema kuwa kamisheni hiyo ina wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la idadi ya Waislamu hao ambao wanatumia njia hatari wakikimbia ukatili na mauaji nchini Myanmar.  

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa tangu mwezi Agosti hadi sasa Waislamu wa jamii ya Rohingya zaidi ya 200 ambao walikuwa na lengo la kufika nchini Bangladesh kupitia  mpaka wa majini wa mto Naf kati ya nchi hiyo na Myanmar, wameghiriki na kufariki dunia. 

Waislamu wa Rohingya wakivuka maji kuelekea Bangladesh 

Msemaji wa UNHCR ameongeza kuwa, wakimbizi waliodhulumika wa Myanmar hawana fedha wala suhula zinazohitajika na hivyo wanalazimika kutumia vifaa hatari kama magogo ya miti yanayoelea ili kuwavusha  katika njia hiyo ya majini ya mpakani kati ya Myanmar na Bangladesh, hatua ambayo inasababisha ajali nyingi za kughariki baharini.